RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema ujenzi wa mindombinu ya elimu nchini unalengo la kuberesa sekta ya elimu iliyoko kwenye mageuzi makubwa ya maendeleo.
Dk. Mwinyi ameyasema hayo alipofungua skuli ya Sekondari Hassan Khamis Hafidhi iliopo Mtopepo, Shehiya ya Munduli Wilaya ya Magharibi A, Mkoa wa mjini Mgharibi, ikiwa ni mwendelezo wa shamrashamra za maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar.
Rais Dk. Mwinyi amesema, nia ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kupunguza msongamano wa wanafunzi wengi madarasani na kubakisha wastani wa wanafunzi 45 kwa kila darasa moja, sambamba na kuweka mkondo mmoja kwa skuli zote za Unguja na Pemba.
Dk. Mwinyi pia alisema hali hiyo itasaidia matokeo mazuri kwa kuwepo mazingira mazuri ya kujifunzia.
Akizungumzia mafanikio makubwa yanayoendelea kupatikana kwenye sekta ya elimu, Rais Dk. Mwinyi ameeleza Sekta hiyo imevuka malengo ya Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM 2021/ 2025 kwa kuboresha miundombinu ya kisasa, zikiwemo Makataba, madarasa yenye ubora wa hali ya juu, maabara madawati, kuboeshwa kwa maslahi ya walimu sambamba na kuongeza ajira za walimu wa hesababati na sayansi, Unguja na Pemba.
Aidha, Rais Dk. Mwiniyi aliushukuru uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kwa kufanikisha vyema miradi yote za Serikali inayosimamiwa na Wizara hiyo kwa kuifanikisha kwa mafanikio makubwa.
Alisema, mradi wa Skuli ya Hassan Khamis Hafidh licha ya kukabiliwa na changamoto kadhaa wakati wa utekelezaji wake hatimae, umefanikishwa kwa mafanikio makubwa nakuongeza kuwa ni mradi pekee uliotekelezwa kwa fedha za uviko 19 kukawia kuzinduliwa hatimae umekamilika ukiwana mafaniko makubwa.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa skuli hiyo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Lela Muhamed Mussa, ameiahidi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kuisimamia kwa ufanisi wa hali ya juu miradi yote inayotekelewa na kusimamiwa na Wizara hiyo.
Pia, Waziri Lela, amemshukuru Rais Dk. Mwinyi na Dk. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa weledi wao wa kuendelea kuusimamia na kuudumisha Muungano wa Tanzania ambao kwasasa unatimiza miaka 60 tokea kuasisiswa kwake mwaka 1964.
Naye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Khamis Abdalla alisema ujenzi wa Skuli ya Sekondari ya Hassan Khamis Hafidh wa ghorofa tatu ulinza mwezi Februari mwaka 2022 hadi uliposuasua mwezi wanane mwaka huo na baadae kukabidhiwa Chuo cha mafunzo kwaajili ya kuuendeleza hadi kukamilika kwake.
Aidha, Katibu huyo amesema ujenzi wa skuli hiyo umejumuisha madarasa 41, ofisi nne za walimu, ofisi ya mwalimu mkuu, vyoo 52, maktaba, maabara, chumba cha kompyuta na stoo, na ukumbi mkubwa wa mikutano.
Akizungumza kwenye hafla hiyo kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi, CCM, Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Magharibi kichama, Muhamed Rajab Sudi alisifia uongozi wa Rais Dk. Mwinyi na kuuelezea sio uongozi wa kujionesha bali ni wakuwatumikia wananchi kwa vitendo kama ambavyo mageuzi makubwa ya maendeleo yanavyoonekana nchi nzima chini ya kipindi kifupi cha uongozi wake.
🔰𝐀𝐒𝐀𝐍𝐓𝐄𝐍𝐈 𝐒𝐀𝐍𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈 𝐖𝐀 𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎!
01-06-2026
𝐒𝐇𝐔𝐋𝐄 𝐘𝐀 𝐌𝐒𝐈𝐍𝐆𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐒𝐀𝐃𝐀𝐋𝐀 𝐘𝐀𝐎𝐍𝐃𝐎𝐀 𝐊𝐄𝐑𝐎 𝐘𝐀 𝐊𝐔𝐓𝐄𝐌𝐁𝐄𝐀 𝐊𝐈𝐋𝐎𝐌𝐄𝐓𝐀 𝟏𝟐 𝐊𝐖𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐈
01-06-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀 𝐀𝐀𝐍𝐙𝐀 𝐙𝐈𝐀𝐑𝐀 𝐖𝐈𝐋𝐀𝐘𝐀𝐍𝐈 𝐇𝐀𝐈, 𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎
01-06-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀 𝐀𝐀𝐍𝐙𝐀 𝐙𝐈𝐀𝐑𝐀 𝐖𝐈𝐋𝐀𝐘𝐀 𝐘𝐀 𝐇𝐀𝐈 𝐌𝐊𝐎𝐀 𝐖𝐀 𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎
01-06-2026
𝐍𝐈 𝐌𝐔𝐃𝐀 𝐖𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐇𝐀𝐈-𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎 𝐒𝐀𝐒𝐀
01-06-2026
𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐌𝐏𝐀 𝐁𝐀𝐉𝐀𝐉𝐈 𝐌𝐊𝐀𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐒𝐈𝐇𝐀 𝐌𝐖𝐄𝐍𝐘𝐄 𝐔𝐋𝐄𝐌𝐀𝐕𝐔 𝐖𝐀 𝐌𝐈𝐆𝐔𝐔
01-06-2026
MAWENZI YAVUNJA REKODI: MITUNGI 3,313 YA OKSIJENI YAZALISHWA KWA MIEZI 6, ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 126 ZAOKOLEWA!
01-06-2026
MAFURIKO YA WANANCHI WA SIHA KWENYE MKUTANO MKUBWA WA HADHARA
01-06-2026
MAPOKEZI YA KATIBU MWENEZI WA CCM NDUGU KENANI L KIHONGOSI MKOANI KILIMANJARO
01-06-2026
🔰 𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈 𝐀𝐖𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐊𝐈𝐒𝐇𝐈𝐍𝐃𝐎 𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎
01-06-2026
CCM INAWATAKIA HERI YA SIKUKUU YA EID AL ADHA
01-06-2026
🔰VYAMA VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA VYAIMARISHA MSHIKAMANO, DKT. DIMWA AHITIMISHA MAFUNZO MAALUM
01-06-2026
KATIBU WA NEC, ITIKADI, UENEZI NA MAFUNZO CCM TAIFA NDUGU KENANI KIHONGOSI AMNADI MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ISIMANI EMMANUELA KAGANDA MTATIFIKOLO
01-06-2026
MUENDELEZO WA MAFUNZO YA VIONGOZI KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE – KIBAHA
01-06-2026
SIKU YA KWANZA YA MAFUNZO KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE LEADERSHIP SCHOOL.
01-06-2026
UFUNGUZI WA MAFUNZO YA VYAMA SITA RAFIKI VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA
01-06-2026
MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA MJUMBE WA KAMATI KUU YA CPC, KOMREDI LIU HAIXING IKULU DAR ES SALAAM
01-06-2026
KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CCM
01-06-2026
CCM NA FRELIMO KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIUCHUMI
01-06-2026
UZINDUZI WA JENGO LA MAKAO MAKUU YA ULINZI WA TAIFA
01-06-2026