Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


Wasira: Idadi ya Wanachama wa CCM Yatosha Kuendelea Kushika Dola 

alternative

 

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Stevin Wasira, amesema idadi kubwa ya wanachama waliosajiliwa ndani ya chama hicho inatosha kukifanya CCM kuendelea kushika dola na kubaki madarakani.  

Wasira alitoa kauli hiyo leo, Januari 23, 2025, baada ya kupokewa na wanachama wa CCM katika Makao Makuu ya chama hicho, jijini Dodoma. Akizungumza mbele ya mamia ya wanachama waliojitokeza, Wasira alisema, "Kwa mtaji wa wanachama tuliowasajili, CCM ina nguvu ya kuendelea kushika madaraka na kuleta maendeleo endelevu kwa Watanzania."  

Akiwa kwenye mkutano huo, Wasira aliwakumbusha wanachama na viongozi kuwa mwaka 2025 ni mwaka muhimu wa uchaguzi wa Rais, Wabunge, na Madiwani, na hivyo aliwataka wanachama waendelee kuwa imara na kushirikiana kuhakikisha chama kinapata ushindi wa kishindo.  

"Huu ni mwaka wa uchaguzi, ni lazima tuhakikishe tunadumisha mshikamano, tukitekeleza sera zetu kwa ufanisi, na kuendelea kuwahudumia Watanzania kwa uadilifu," alisisitiza Wasira.

alternative
Habari Nyingine