Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
MWENEZI MAKALLA APIGILIA MSUMARI SUALA LA MITANO TENA LIWE KWA MAMA SAMIA PEKEE, WENGINE WAFUATE UTARATIBU .
Katibu wa NEC - Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa Ndugu. Amos Makalla ambaye pia ni Mlezi wa Mkoa wa Dar es salaam (kichama) akizungumza katika Ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo Leo amepokelewa na Umati wa WanaCCM . Mwenezi Makalla amesema Kumezuka suala la Watu kupigiana chapuo yaani "... unakuta Wilaya nzima wanakuwa na ajenda na Mtu, wanaimba Mitano tena kwa Diwani ama Mbunge kumbe ni ajenda, na wanaacha kabisa Chama, unakuta anapigiwa chapuo mtu mmoja, sasa nami nielekeze suala hili la Mitano tena liwe kwa Mwenyekiti wetu, wengine tufuate Utaratibu kwani ndivyo tulivyowekeana Taratibu."
06 Julai 2024 Mapokezi ya Mlezi wa Mkoa wa Dar es salam na Katibu Mwenezi wa CCM Taifa
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.