Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
WAZIRI AWESO AMUHAKIKISHIA KATIBU MKUU DKT. NCHIMBI KUPELEKA MILIONI 400 WILAYANI NKASI KUKAMILISHA MRADI WA MAJI
Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amempigia simu Waziri wa Maji Ndugu. Jumaa Aweso , na kumtaka kutolea majibu kuhusu ni lini fedha Tsh Milioni 400 zitatolewa ambazo zilizotakiwa kupelekwa Nkasi kwa ukamilishaji wa mradi wa maji wenye thamani ya Tsh Milioni 700 ambapo hadi sasa zimetolewa Milioni 300 pekee.
Katika majibu yake aliyotoa katika mkutano wa hadhara kwa njia ya simu, Waziri Aweso amemuhakikishia Balozi Dkt. Nchimbi kuwa hadi kufikia kesho tarehe 15 Aprili, 2024 fedha hizo Tsh Milioni 400 zitakuwa zimetolewa.
Vilevile, Waziri Aweso amesema Wizara ya Maji itaendelea kutekeleza dhamira ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kumtua Mama ndoo kichwani na wakati wote kutekeleza maagizo ya CCM kwa kuzingatia utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020/2025.
Naye, Balozi Dkt. Nchimbi amempongeza Waziri Aweso kwa hatua hiyo.
" Katika wizara zinazogusa misingi ya wananchi basi Rais wetu Mhe. Dkt. Samia amefanya uteuzi kwa umakini zaidi ndio maana Aweso ni mnyenyekevu na mchapakazi wa kweli " Alisema Balozi Dkt. Nchimbi
Aidha, Balozi Dkt. Nchimbi amewahaidi wananchi wa Nkasi kuwa atazungumza na Waziri wa Afya Ndugu. Ummy Mwalimu kuhakikisha changamoto ya uhaba wa wauguzi Wilayani humo linafanyiwa kazi na kuongezwa kwa wauguzi ili kusudi Wananchi wa Nkasi kuendelea kufurahia kupata huduma bora ya Afya.
📍 Nkasi - Rukwa
🗓️ 14 Aprili, 2024
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.