Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Askari wa Tanzania kupata Mafunzo nchini Urusi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amesema serikali kupitia wizara imeamua kuunganisha na kuimarisha mahusiano na nchi ya Urusi katika masuala mbalimbali ikiwemo kubadilishana uzoefu sambamba na askari wa vyombo vya ulinzi kwenda nchini Urusi kujifunza njia mbalimbali za kudhibiti uhalifu katika vyuo vilivyopo nchini humo.
Ameyasema hayo wakati wa mazungumzo ya kujadili hatua hizo ambapo amekutana na viongozi watatu kutoka serikali ya Urusi kwa nyakati tofauti akiwemo katibu wa baraza la usalama la shirikisho la Urusi Nikolai Patrushev,Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wa Serikali ya Urusi,Igor Zubov na Mkuu wa Usalama wa Taifa wa Serikali ya Urusi,Sergey Beseda.
‘Nimefanya mazungumzo na viongozi watatu kutoka serikali ya Urusi,mazungumzo yalijikita hasa katika masuala ya kudhibiti uhalifu katika mkondo wa matumizi ya teknolojia kuna mambo tumeyazungumza sasa tutarudi nyumbani na kukaa na timu za wataalamu kutoka katika Vyombo vya Ulinzi vilivyopo chini ya wizara lakini pia tumeona haja ya askari wetu kuja kusoma katika vyuo vya huku vinavyofundisha masuala ya usalama tukiamini watakapomaliza masomo na mafunzo yao watakuja kuwa msaada mkubwa kwa nchi katika sekta hiyo ya ulinzi na usalama.’alisema Waziri Masauni
Aligusia pia masuala ya usalama barabarani ambapo pia matumizi ya teknolojia hayaepukiki katika kudhibiti ajali za barabarani ambazo zimekua zikiacha vilio na simanzi kwa ndugu wanaopoteza wapendwa wao huku akiahidi kujumuisha masuala ya usalama barabarani katika mipango na programu mbalimbali watakazoingia makubaliano na nchi ya Urusi sambamba na huduma za kiuhamiaji katika viwanja vya ndege nchini.
‘Matumizi ya teknolojia katika karne hii ni suala ambalo haliepukiki kwanza linaondoa kero na malalamiko mengi pia hata masuala ya mapato yanakua na njia rasmi tofauti na ilivyo sasa,tunataka kupunguza na kuondoa ajali za barabarani ambazo zimekua na madhara makubwa nchini kwetu,tunaamini teknolojia ikiwemo matumizi ya kamera za usalama barabarani zinaenda kutibu matatizo sugu yanayosababisha ajali ambazo upelekea vifo lakini pia ukiangalia wenzetu katika viwanja vya ndege huduma za uingiaji na utokaji nchini zimerahisishwa kutokana na matumizi ya teknolojia hakuna mistari mirefu tena sasa na hilo suala pia tunaenda kuliangalia.’ Aliongeza Waziri Masauni
Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika vikao hivyo viongozi hao wa serikali ya urusi waliahidi kushirikiana na serikali ya Tanzania katika programu mbalimbali watakazokubaliana ikiwemo udhibiti wa uhalifu wa kimtandao,matishio ya ugaidi na uboreshaji wa teknolojia ya kudhibiti uhalifu wa aina mbalimbali.
Waziri Masauni yupo nchini Russia kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Maafisa wa Daraja la Juu kutoka Serikalini wanaohusika na Mambo ya Usalama ambapo mkutano huo unafanyika katika Jiji la St. Petersburg, ambapo takribani nchi 20 zimehudhuria mkutano huo.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.