RAIS Dk. Hussein Ali Mwinyi, ametoa wito kwa Wahandisi wanawake kushirikiana na kuhakikisha wanachangia vilivyo maendeleo ya nchi kufikia malengo ya kuwa na uchumi wa juu, wa kati ifikapo mwaka 2025.
Dk. Mwinyi alitoa wito huo kwenye ufunguzi wa Kongamano la nane la Wahandisi wanawake, ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Alisema, Serikali za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Mapinduzi ya Zanzibar, zinatambua na kuthamini mchango wa Wahandisi wanawake nchini kutokana na kazi za uhandisi wanazozifanya.
Alisema, Makangamano kama hayo yamekuwa na mchango mkubwa wa kuunga mkono juhudi za Serikali za kuendeleza ubunifu wa sanyansi na kuleta chachu ya maendeleo ya Taifa ikiwemo ujenzi wa viwanda.
Dk. Mwinyi aliongeza, Serikali zote mbili zinajitahidi kushirikisha wanawake kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo kwa kuwawekea mazingira wezeshi ya kujiajiri, kuhamasisha utambuzi wa fursa mbalimbali kupitia rasilimali zilizopo nchini, kurejesha stadi za ujuzi, elimu ya uanagenzi vyuoni na kutenga bajeti kwa ajili ya kufanikisha shughuli za utafiti na ubunifu wa fani tofauti.
Alisema, fani ya uhandisi ina umuhimu mkubwa kwa ustawi wa nchi pia ni uti wa mgongo wa shughuli nyingi za kiuchumi. Hivyo aliwataka vijana na wanawake kuzitumia fursa ziliopo ili kuyafikia malengo yao.
Pia, aliwashauri wahandisi wanawake kufungua kampuni na kujiajiri kupitia ukandarasi na uhandisi nakueleza hatua hiyo itachangia sana maendeleo ya nchi kwa kujenga miundombinu imara itakayodumu kwa muda uliokusudiwa.
Aidha, alieleza kutokana na idadi ndogo ya wahandisi iliopo nchini, Serikali za SMZ na SMT zinaendelea kuweka mipango madhubuti ya kuongeza idadi ya wahandisi wanawake na mafundi sanifu pamoja na kuhakikisha wanasaidiwa vizuri wasichana wanaosoma masomo ya Sayansi katika elimu za Sekondari, vyuo vya mafunzo ya amali na vyuo vikuu, hatua ambayo bila shaka itasaidia kuongeza idadi ya wahandisi wanawake nchini.
Hata hivyo, alihimiza ushirikiano baina ya wahandisi wanawake wa Zanzibar na Kitengo cha Taasisi ya Wahandisi Tanzania Bara kwa madhumuni ya kuendeleza sekta ya uhandisi nchini Tanzania.
Akizungumza kwenye kongamano hilo kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Prof. Makame Mnyaa Mbarawa, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Mhandisi Aisha Amour alisema Serikali inatambua mchango wa wahandisi katika kukuza uchumi wa taifa uanzishwaji wa viwanda mbalimbali.
Naye, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Dk. Khalid Salum Muhamed alieleza kongamano la nane la wahandisi wanawake linaloendelea visiwani Zanzibar litaongeza hamasa na uelewa kwa vijana na kuwashajihisha zaidi wanafunzi kuendelea kupenda masomo ya sayansi ili kujijengea kada zenye tija na utaalamu, kwani bado mahitaji ya wahandisi wanawake bara na Zanzibar yanahitajika.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa taasisi ya wahandisi Tanzania, kitengo cha wanawake, Rihanna Juma aliisihi jamii kuachana na mitazamo potofu juu ya wahandisi wanawake kwa kuangalia mapungufu yao yanayotokana maumbile ya jinsia zao zikiwemo uzazi na uhalisia wao, hivyo aliwataka waajiri kuona umuhimu wao na kutambua mchango wao kwa maendeleo ya taifa kwa kuwatumia kwenye kazi za vitendo badala ya kuwapa kazi za ofisini pekee.
KIPINDI MAALUMU
09-06-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐀𝐒𝐈𝐌𝐀𝐌𝐈𝐒𝐇𝐀 𝐌𝐒𝐀𝐅𝐀𝐑𝐀 𝐊𝐔𝐒𝐀𝐋𝐈𝐌𝐈𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈 𝐍𝐀 𝐊𝐈𝐉𝐈𝐖𝐄 𝐂𝐇𝐀 𝐂𝐇𝐀𝐃𝐄𝐌𝐀 𝐀𝐑𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐌𝐉𝐈𝐍𝐈
09-06-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐀𝐓𝐄𝐌𝐁𝐄𝐋𝐄𝐀 𝐊𝐈𝐓𝐔𝐎 𝐂𝐇𝐀 𝐀𝐅𝐘𝐀 𝐊𝐀𝐋𝐎𝐋𝐄𝐍𝐈, 𝐀𝐑𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐌𝐉𝐈𝐍𝐈
09-06-2026
𝐀𝐑𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐘𝐀𝐀𝐌𝐁𝐈𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐂𝐇𝐀𝐆𝐔𝐀 𝐌𝐀𝐄𝐍𝐃𝐄𝐋𝐄𝐎 𝐁𝐀𝐃𝐀𝐋𝐀 𝐘𝐀 𝐌𝐀𝐀𝐍𝐃𝐀𝐌𝐀𝐍𝐎
09-06-2026
𝐌𝐀𝐏𝐎𝐊𝐄𝐙𝐈 𝐘𝐀 𝐊𝐀𝐓𝐈𝐁𝐔 𝐖𝐀 𝐍𝐄𝐂, 𝐈𝐓𝐈𝐊𝐀𝐃𝐈, 𝐔𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐍𝐀 𝐌𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐎 𝐂𝐂𝐌, 𝐍𝐃𝐔𝐆𝐔 𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐋𝐀𝐁𝐀𝐍 𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈, 𝐎𝐅𝐈𝐒𝐈 𝐙𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐖𝐈𝐋𝐀𝐘𝐀 𝐘𝐀 𝐀𝐑𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐌𝐉𝐈𝐍𝐈
09-06-2026
𝐒𝐀𝐒𝐀 𝐍𝐈 𝐀𝐑𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐌𝐉𝐈𝐍𝐈, 𝐌𝐖𝐄𝐍𝐃𝐎 𝐌𝐃𝐔𝐍𝐃𝐎!
09-06-2026
𝐀𝐑𝐔𝐌𝐄𝐑𝐔 𝐘𝐀𝐒𝐈𝐊𝐈𝐀 𝐖𝐈𝐓𝐎 𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐋𝐈𝐍𝐃𝐀 𝐌𝐀𝐀𝐃𝐈𝐋𝐈 𝐍𝐀 𝐇𝐀𝐊𝐈 𝐙𝐀 𝐖𝐀𝐓𝐎𝐓𝐎
09-06-2026
𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐀𝐒𝐀𝐌𝐁𝐀𝐙𝐀 𝐔𝐏𝐄𝐍𝐃𝐎 𝐖𝐀 𝐀𝐆𝐀𝐏𝐄 𝐊𝐖𝐄𝐍𝐘𝐄 𝐊𝐈𝐉𝐈𝐖𝐄 𝐂𝐇𝐀 𝐂𝐇𝐀𝐃𝐄𝐌𝐀 𝐀𝐑𝐔𝐌𝐄𝐑𝐔
09-06-2026
𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈 𝐀𝐀𝐍𝐙𝐀 𝐙𝐈𝐀𝐑𝐀 𝐀𝐑𝐔𝐌𝐄𝐑𝐔 𝐊𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐊𝐀𝐆𝐔𝐀 𝐔𝐇𝐀𝐈 𝐖𝐀 𝐂𝐇𝐀𝐌𝐀
09-06-2026
𝐌𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐎 𝐖𝐀 𝐇𝐀𝐃𝐇𝐀𝐑𝐀 𝐖𝐀 𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀 𝐖𝐈𝐋𝐀𝐘𝐀 𝐘𝐀 𝐊𝐀𝐑𝐀𝐓𝐔 - 𝐌𝐊𝐎𝐀 𝐖𝐀 𝐀𝐑𝐔𝐒𝐇𝐀
09-06-2026
𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐓𝐔𝐍𝐔𝐊𝐈𝐖𝐀 𝐒𝐇𝐀𝐇𝐀𝐃𝐀 𝐘𝐀 𝐇𝐄𝐒𝐇𝐈𝐌𝐀 𝐔𝐑𝐔𝐒𝐈
09-06-2026
𝐀𝐑𝐔𝐌𝐄𝐑𝐔, 𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐀𝐍𝐀𝐊𝐔𝐉𝐀!
09-06-2026
𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐑𝐀𝐒𝐌𝐈 𝐔𝐑𝐔𝐒𝐈, 𝐀𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐀 𝐍𝐀 𝐏𝐔𝐓𝐈𝐍
09-06-2026
𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎, 𝐓𝐔𝐍𝐀𝐊𝐔𝐉𝐀
09-06-2026
𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐃𝐊𝐓. 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐖𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈 𝐌𝐎𝐒𝐂𝐎𝐖, 𝐔𝐑𝐔𝐒𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐙𝐈𝐀𝐑𝐀 𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀
09-06-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀 𝐀𝐖𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈 𝐖𝐈𝐋𝐀𝐘𝐀 𝐘𝐀 𝐒𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐈𝐑𝐎 𝐊𝐖𝐀 𝐙𝐈𝐀𝐑𝐀 𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐊𝐀𝐙𝐈
09-06-2026
𝐅𝐔𝐍𝐆𝐀 𝐊𝐀𝐙𝐈 𝐌𝐊𝐎𝐀 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐍𝐘𝐀𝐑𝐀 𝐋𝐄𝐎!!!
09-06-2026
𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈 𝐀𝐓𝐄𝐌𝐁𝐄𝐋𝐄𝐀 𝐒𝐇𝐈𝐍𝐀 𝐍𝐀. 𝟐 𝐊𝐀𝐓𝐀 𝐘𝐀 𝐁𝐎𝐍𝐆𝐀
09-06-2026
𝐁𝐀𝐁𝐀𝐓𝐈 𝐌𝐉𝐈𝐍𝐈 𝐋𝐄𝐎 𝐓𝐔𝐍𝐀𝐈𝐅𝐔𝐍𝐈𝐊𝐀!!!
09-06-2026
𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈 𝐀𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐀 𝐍𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈 𝐇𝐀𝐍𝐀𝐍𝐆, 𝐀𝐒𝐈𝐊𝐈𝐋𝐈𝐙𝐀 𝐍𝐀 𝐊𝐔𝐓𝐀𝐓𝐔𝐀 𝐊𝐄𝐑𝐎 𝐙𝐀𝐎
09-06-2026