Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
KINANA AFUNGUA MAFUNZO
KUWAJENGEA UWEZO VIONGOZI WANAWAKE KUTUMIA TAKWIMU
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana amefungua mafunzo kwa viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa ngazi mbalimbali.
Kinana amefungua mafunzo hayo leo Mei 25, 2024 yakiwa yanahusu matumizi ya takwimu zilizotokana na sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 katika kupanga mipango ya maendeleo ya wananchi.
Lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha viongozi hao kupanga mipango ya maendeleo ya wananchi katika sekta mbalimbali ili kuhakikisha rasilimali za taifa zinatumika kwa ufasaha.
Mafunzo hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Mwenyekiti wa UWT Taifa Mary Pius Chatanda, Katibu Mkuu wa UWT, Suzan Kunambi na Kamisaa wa Sensa, Spika Mstaafu Anne Makinda.
Pamoja na viongozi wa UWT, wengine walioshiriki katika mafunzo hayo ni wabunge wanawake wa CCM, watendaji wanawake wa CCM kutoka Jumuiya ya Wazazi na wenyeviti wanawake wa CCM wa Mikoa na wilaya.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.