CCM INATAMBUA UWEPO WA BARAZA LA WAZEE KWA KUWA NI CHOMBO CHA USHAURI MZURI - NDG. GAVU
Katibu wa NEC, Oganaizesheni wa CCM Taifa Ndugu. Issa Haji Gavu, amesema kuwa kuna umuhimu wa kuendelea kusisitiza vikao kuanzia ngazi ya mashina pamoja na vikao vya baraza la wazee ambavyo vitasaidia kupata idadi ya wanachama na kujenga utamaduni wa kutafuta majawabu dhidi ya changamoto zinazowakabili.
“ Katiba inaelekeza kila kipindi cha miezi mitatu, balozi anapaswa kufanya kikao cha wananchama wake. Makatibu wa mikoa mnapaswa kusimamia utekelezaji wake. Kwa ngazi ya tawi katiba inaturuhusu kufanya vikao vya wanachama wote kupata nafasi ya kufanya tathimini ya nguvu zetu na changamoto zinazotukabili” alisema Ndugu. Gavu
Pia, Ndg. Gavu amesema Katiba ya CCM inatambua uwepo wa Baraza la Wazee la CCM ambalo ni chombo cha ushauri, kuelekeza, kuonya na kutafuta jawabu la changamoto kwa busara, heshima na uzoefu.
" CCM tunatambua na kuamini katika baraza la wazee kwakuwa wamekuwa sehemu ya chombo kizuri cha kutoa ushauri mzuri wenye kujenga na kuelekeza, lakini wamekuwa sehemu ya kusaidia kwenye kuonya na kutafuta jawabu la changamoto kwa kutumia hekima zao kubwa, busara , heshima na udhoefu walionao "
ποΈ22 Aprili, 2024
πMbinga - Ruvuma