DKT. NCHIMBI AZINDUA KIWANDA CHA TANGA CABLE INDUSTRIES
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Balozi Ndg. Dkt. Emmanuel Nchimbi leo Juni 8,2024 akiwa katika siku ya pili ya ziara yake mkoani Tanga amezindua kiwanda cha Tanga cable industries kilichopo Tanga mjini.
Katika ziara hii Dk Nchimbi ameambatana na Katibu wa NEC-Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndg. Amosi Makalla, Katibu wa NEC-Organaizesheni Ndg. Issa Ussi Haji (Gavu) pamoja na Katibu wa NEC- Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg. Rabia Abdallah Hamid.