MONGELA ASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI 2024
Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara Ndg.John V. K Mongela ameshiriki Maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani,
huku kauli Mbiu ya Maadhimisho hayo ikiwa ni "Urejeshwaji wa Ardhi,Ustahimilivu wa Hali ya Jangwa na Ukame"
Aidha Mongela alitoa salamu za CCM kwa kuipongeza Serikali kwa kutekeleza Ilani ya CCM kwa vitendo hususani kwenye suala la kutunza Mazingira na upandwaji wa miti.
Naibu katibu Mkuu ameyasema hayo tarehe 05 Juni,2024 kwenye ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Mkoani Dodoma.