Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Rais Samia Suluhu Hassan atoa Mhadhara wenye Mada ya Falsafa ya R Nne (4Rs) ambayo anaitumia katika kuongoza Serikali ya Awamu ya Sita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Amiri Jeshi Mkuu na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa Mhadhara wenye Mada ya Falsafa ya R Nne (4Rs) ambayo anaitumia katika kuongoza Serikali ya Awamu ya Sita. Mhadhara huo umefanyika katika Chuo Cha Taifa Cha Ulinzi (NDC),Kunduchi Jijini Dar es Salaam tarehe 26, Juni 2024. Falsafa yake ya R4 ni: Reconciliation(Maridhiano), Resilience(Ustahimilivu), Reforms(Mageuzi) and Rebuilding (Kujenga upya).
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.