Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
DKT NCHIMBI AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MWANDOYA-KISESA
Wananchi wa Kata ya Mwandoya, Jimbo la Kisesa, Wilaya ya Meatu, mkoani Simiyu, wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, alipokuwa akizungumzia masuala na hoja mbalimbali kutoka kwa wawakilishi wao, Ndugu Basu Kayungilo, Diwani wa Kata ya Mwandoya na Ndugu Luhaga Mpina, Mbunge wa Kisesa, leo tarehe 7 Oktoba 2024. Balozi Nchimbi alisimama Mwandoya kuwasalimia wakazi wa eneo hilo na kuzungumza nao masuala ya maendeleo yanayohusu jimbo hilo la Kisesa, akiwa njiani kuelekea Mwanhuzi, Meatu, ambapo ni mwendelezo wa ziara yake ya siku 3, mkoani humo.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.