Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Katibu Mkuu Balozi Dk Emmanuel John Nchimbi, akizungumza na Wanachama wa CCM, wawakilishi wa makundi mbalimbali, Viongozi wa Chama na Jumuiya zake wa ngazi mbalimbali, kwenye mkutano wa ndani Kilimanjaro,
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk Emmanuel John Nchimbi, akizungumza na Wanachama wa CCM, wawakilishi wa makundi mbalimbali, Viongozi wa Chama na Jumuiya zake wa ngazi mbalimbali, kwenye mkutano wa ndani, uliofanyika Ofisi za CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Jumatano Juni 5, 2024, ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya kikazi mkoani humo, ambayo ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Oganaizesheni, Ndugu Issa Usi Haji Gavu, Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Ndugu Amos Gabriel Makalla na Ndugu Rabia Hamid Abdalla, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI).
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.