Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
SERIKALI YA CCM ITAENDELEA KUNUNUA CHAKULA KWA WAKULIMA WETU - BALOZI DKT. NCHIMBI
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kuhakikisha serikali inaendelea kununua mazao ya vyakula kutoka kwa wakulima wake wa ndani kwa bei zenye kuwanufaisha wakulima wote.
Dkt. Nchimbi amesema kununua vyakula kutoka kwa wakulima wetu wa ndani kutasaidia katika kudhibiti unyonyaji kwa wakulima na mfumuko wa ongezeko la bei.
" Chama Cha Mapinduzi tutahakikisha Maghala ya taifa ya serikali yanaendelea kununua chakula kwa wakulima wetu wa ndani ili kuhakikisha wanaendelea kuthibiti unyonyaji wa bei ya manunuzi kwa wakulima na kutokuwepo kwa mfumuko wa bei, pia tutahakikisha wakulima wanalipwa kwa wakati na wale ambao bado wanadai niwahakiishie kuwa nimeshaongea na Waziri wa Kilimo Ndugu. Hussein Bashe amenihakikishia kuwa hadi kufikia wiki ijayo malipo hayo yatakuwa yamekwishalipwa "
" CCM kwa kutambua dhamana yake kwamba ni chama kinachotokana na wananchi, kitaendelea kuhakikisha serikali inatenda mambo yanayotarajiwa na wananchi , inaimarisha usalama wa raia na mali zao, inatoa huduma bora kwa sekta ya afya, inatengeneza miundombinu rafiki ya barabara na sekta nzima ya usafirishaji na mengine yote kwa sekta mbalimbali "
Aidha, Balozi Dkt. Nchimbi amewapongeza wananchi wa mkoa wa Ruvuma kwakuwa kati ya mikoa 5 inayoongoza kutoa huduma ya chakula nchini kwa ziaid ya miongo minne na hii inadhiirisha wazi ya kuwa wananchi wa Ruvuma ni wachapakazi.
🗓️20 Aprili, 2024
📍Songea Mjini - Ruvuma
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.