MKUTANO MKUU CCM TAIFA KAZI NA DAWA
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, akifurahia burudani ya muziki pamoja na Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Taifa, wakati vikundi mbalimbali vya sanaa ya vilipokuwa vikitumbuiza kabla ya kikao kuanza rasmi, leo Ijumaa, tarehe 30 Mei 2025.
Mkutano huo ulianza jana Alhamis, tarehe 29 Mei 2025, katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma, na kumalizika leo ambapo mojawapo ya agenda ni uzinduzi wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2025 - 2030.
#KazinaUtuTunasongaMbele
#SafariyaUshindi2025