Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


HATUWEZI KUIKOSOA SERIKALI KAMA SISI WENYEWE HATUWEZI KUTIMIZA WAJIBU WETU - KATIBU MKUU DKT. NCHIMBI

alternative

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Ndugu. Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amewataka Viongozi mbalimbali wa CCM kwa ngazi zote kutimiza wajibu wao ipasavyo.

Balozi Dkt. Nchimbi amesema Chama Cha Mapinduzi kina jumla ya mashina 246,000 na kila shina lina viongozi 5 ambapo inapelekea kuwa na zaidi ya Viongozi Milioni 1 katika ngazi hiyo na kutokana na uwepo wa Viongozi wao, Hivyo kwa kuambatana na Viongozi wengine wa sekretarieti ya CCM Taifa wamefika ili kuona ufanisi wa kazi kwa Viongozi kuanzia Mashina hadi Mkoa kwakuwa uwepo wa ufanisi mzuri wa kazi zao ndio unaweza kuwafanya kuweza kuikosoa serikali na kutoa ushauri na muongozo kwa maslahi mapana ya Watanzania.

" Hatuwezi kuikosoa serikali tunayoiongoza kama sisi wenyewe hatuwezi kutimiza wajibu wetu "

" Ndio maana tumeanza kujikagua wenyewe kisha tuwe na ujasiri wa kuikosoa serikali, sasa nawapongeza shina namba tana la paraides pale majengo, mnaifanya kazi yenu vizuri sana. "

Alisema Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi
Katibu Mkuu wa CCM

Ameyasema hayo kwenye Mkutano wa kueleza muelekeo wa Chama pamoja na mambo mengine kuhusu uelekeo wa uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka huu wa 2024 na uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Mkutano huu umekutanisha, Wajumbe wa Mashina na Wenyeviti wa  Mitaa, Vijiji na  Vitongoji na Miitaa, Viongozi wa Chama ngazi zote, Wazee mashuhuri, Viongozi wa Dini pamoja na Watendaji wa serikali ngazi zote na Taasisi zisizo za kiserikali.

🗓️ 13 Aprili, 2024
📍Mpanda - Katavi

alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine

Nukuu za Viongozi