CCM TUMEIMARIKA ZAIDI - DK. DIMWA
CHAMA Cha Mapinduzi(CCM)Zanzibar kimewataka watendaji wake kujiimarisha na mabadiliko ya mienendo ya hali ya siasa inavyokwenda.
Akizungumza katika ziara ya sekretarieti ya Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM,Zanzibar mkoa wa Kaskazini Unguja,Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Zanzibar Dk. Mohammed Said Mohammed 'Dimwa'.
Naibu Katibu Mkuu huyo alisema CCM pamoja na jumuiya zake zinapaswa kujithatiti,kujijenga na kujijenga kuwa na uwezo mpya wa kulingana na uzito wa mapambano ya kisiasa yaliyopo.
"Siasa zetu zimeanza kubadilika sana na wala si siasa za kwenye majukwaa hivi karibuni juzi ACT-Wazalendo walisema tunamsubiri Dk.Dimwa ajibu hoja nasema tutajibu hoja kwa hoja tena tuna joja nyingi za kujibu," alisema
Alisema katika hilo hoja hizo haitaitoa kwenye reli CCM katika kutekeleza ilani ya uchaguzi.
"Wanazungumza suala la ujenzi wa uwanja wa Amani kuwa fedha zinazotoka wapi bila ya kupitishwa na Baraza la Wawakilishi lakini wawakilishi watakuwa wanajua kuwa kuna mfuko wa serikali ambao unaitwa mfuko wa hazina ndio kazi yake hii,"alisema
Naibu Katibu Mkuu huyo alisema yeye ana uzoefu wa suala hilo kutokana na kuwa ameshawahi kuwa Mwakilishi kwa hivyo anatambua jambo hilo na kwamba atawajibu hoja kwa hoja na si kujibu mambo mengine.
Alisema CCM itaendelea kuhubiri amani ili Zanzibar iendelee kubaki na amani na kuachana na maneno ya wapinzani yanayoashiria uvunjifu wa amani.
Pia,alisema, vyama vya siasa muda wote vinatakiwa kuhubiri amani kutokana na kuwa ikitoweka haiwezi kurudi tena, na kwamba CCM itaendelea kuhubiri amani.
"Licha ya kuwa vyama vyengine vya siasa vimekuwa vikihubiri uvunjifu wa amani lakini sisi hatutahubiri masuala hayo na tutaendeleza amani ya nchi iliyopo ili tuweze kupeleka maendeleo kwa wananchi wote bila ya kubagua," alisema.
Alisema CCM itaendelea kujibu hoja kwa hoja ambazo serikali inayoongozwa na CCM imefanya maendeleo ikiwemo, kujenga shule za kisasa za ghorofa.
Mbali na hilo,Naibu Katibu Mkuu huyo aliwataka viongozi wa CCM kuendelea kutangaza maendeleo yanayofanyika kupitia ilani ya uchaguzi ya CCM inavyotekelezeka kwa wananchi.
"Tuna kila sababu ya kutembea kifua mbele, awahamasishe wanaCCM kuyatangaza mafanikio yanayotekelezwa chini ya uongozi wa Rais wa Zanzibar Dk.Hussein Ali Mwinyi,"alisema
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
09-12-2025
RAIS SAMIA AKIWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WATEULE- IKULU CHAMWINO DODOMA
09-12-2025
WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA (GENERAL)
09-12-2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ..
09-12-2025
RAIS SAMIA AKIHUTUBIA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
09-12-2025
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
09-12-2025
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
09-12-2025
π¨ππππ£πππππ πͺπ πππ§. π¦ππ ππ π¨π ππππ§π ππ ππ‘π ππͺπ πͺππ£ππ‘πππ‘π, πͺππππ¨ππππ πππ
πππ©πππͺ ππ πͺπͺ πΏπ π©. πππππ§π€ ππ¬ππ₯π€π ππ πππ€π£ππ€π―π π¬π πΎππΌπΏπππΌ π£π πΌπΎπ
09-12-2025
πππ§. π¦ππ ππ ππ§π¨π π‘πππ‘π π¬π ππ₯πππ π¬π ππππ’π π
09-12-2025
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
09-12-2025
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
09-12-2025
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
09-12-2025
WANACHAMA 280 WA CHADEMA WATIMKIA CCM
09-12-2025
BALOZI NCHIMBI: MAONI YOYOTE KUHUSU AMANI YA TANZANIA HAYATAPUUZWA
09-12-2025
π¦ππ₯πππππ π¬π π₯πππ¦ πππ§. π¦ππ ππ ππ ππͺπππ ππππ π π¬π π πππ‘πππππ’ ππππ π¦ππππ π¨ - ππ£π. ππ π’π¦ π ππππππ
09-12-2025
MAKALLA: BARABARA YA MPWAPWA NJIAPANDA KONGWA KUJENGWA LAMI
09-12-2025
BALOZI NCHIMBI AWASILI ARUSHA
09-12-2025
TAARIFA KWA UMMA
09-12-2025
UCHAGUZI MKUU SIO AJALI-WASIRA
09-12-2025
πͺπππ¨π ππ π π¦ππππππ¨π π©ππ’π‘ππ’ππ ππππππππ ππͺππ‘π¬π ππ¨π₯π ππ π ππ’π‘π - (π ππ) πππ©π¨
09-12-2025