RAIS SAMIA AKIFUATILIA BUNGE LA BAJETI KUU YA SERIKALI YA MWAKA 2024/25
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa Mhe.Samia Suluhu Hassan Pamoja na Wasaidizi wake akifuatilia Bunge la Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2024/25 kwa njia ya runinga nyumbani kwake Chamwino Mkoani Dodoma.Hotuba hiyo ilikuwa ikisomwa bungeni na Waziri wa Fedha, Mhe.Dkt.Mwigulu Lameck Nchemba.