Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongoza Kikao cha Dharura cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongoza Kikao cha Dharura cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
kutekeleza azimio la Mkutano Mkuu kuhusu uteuzi wa wagombea wa nafasi ya Urais kwa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika Uchaguzi
Mkuu wa mwaka 2025. Kikao kilichofanyika leo tarehe 19 Januari 2025 katika ukumbi wa
NEC maarufu kama White House ambapo Wajumbe wamepitisha jina la Dkt. Samia Suluhu
Hassan kwa upande Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa
upande wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.