Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


RAIS DK. HUSSEIN ALI MWINYI AMESEMA AMEDHAMIRIA KUENDELEZA MAGEUZI MAKUBWA YA HUDUMA ZA JAMII NCHINI KUPITIA SEKTA MBALIMBALI.

alternative

Dk. Mwinyi aliyasema hayo kwenye ziara ya kuutembelea mkoa wa Mjini Mgaharibi, kukagua na kuweka mawe ya msingi miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo ujenzi wa nyumba za maendeleo kwenye mji mpya wa Dk. Hussein Mwinyi, Mombasa viwanja vya magereza, unaosimamiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF), ujenzi wa nyumba za makaazi Kwa mchina unazosimamiwa na Shirika la nyumba Zanzibar, Skuli ya Sekondari Mtopepo na Skuli ya Sekondari Mwembeladu, Wilaya ya Mjini.

Alisema, Serikali ya awamu nane imedhamiria kuendeleza ujenga wa skuli za maghorofa kutoka ngazi ya Chekechea, msingi hadi Sekodari, kuboresha mazingira bora ya walimu ikiwemo maslahi yao, kutoa ajira mpya za walimu, kuboresha mitaala ya elimu, kuongeza ufaulu mzuri pamoja na kuondosha zero kwa wanafunzi wa kidato cha nne na sita. Dk. Mwinyi pia alieleza hatua iliyofikiwa na Serikali sasa imepitiliza ahadi ya ilani ya CCM ya 2020 - 2025 ilipoahidi kujenda mabanda 1500 ya skuli za msingi na sekondani wakati hivi sasa kumejengwa Skuli za ghorofa 64 zenye miundombinu ya kisasa ikiwemo vyoo zaidi ya 50 kwa kila skuli, maktaba tatu tatu, maabara, vyumba vya kompyuta (ICT), ofisi bora za walimu na wakuu wa skuli, stoo, vyumba vya kusalia pamoja na ofisi za walinzi.

Akizungumzia makaazi ya kisasa, Rais Dk. Mwinyi amesema awamu ya nane ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imedhamiria kuongeza nyumba nyingi zaidi, za kisasa na za gharama nafuu ili kukidhi haja na uwezo wa wananchi wake wa matabaka yote, pamoja na kujenga miji ya kisasa yenye hadhi na wakati uliopo kwa kuboresha maisha bora wa wananchi. Alisema, ni wakati sasa wa kuondokana na makazi ya kiholela na kuzingatia makaazi na mipango bora ya miji kwa kuiagiza Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Zanzibar kupima na kutoa maeneo yaliyopimwa. Hata hivyo, Rais Dk. Mwinyi alisema Serikali pia imepanga kutoa maeneo mengine zaidi ya ujenzi wa nyumba bora za maendeleo ikiwemo maeneo ya Kwamabata, Chumbuni na maeneo
mengine ya Zanzibar pamoja na kuondosha kodi za ongezeko la thamani kwa wananchi ili kuweka usawa wa watu wake na kumudu kumiliki nyumba hizo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye ziara hiyo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Lela Muhamed Mussa, alisema azma ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kuimarisha Sekta ya elimu nchini ambayo kwasasa imepiga hatua kubwa kuliko matarajio iliyojiwekea awali. Alisema, mafanikio ya elimu Zanzibar yanatokana na juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuimarisha mazingira wezeshi wa mfumo bora wa elimu Zanzibar, ushirikiano baina ya watendaji wa wizara, walimu wazazi, wanafunzi na wadau wa elimu nchini.

Naye, Waziri wa Ardhi na Maendelo, Rahma Kassim Ali, alisifu juhudi za Rais Dk. Mwinyi kwenye miradi ya maendeleo ikiwemo kuboreshwa kwa makazi bora ya nyumba za maenedeleo. Ziara ya Rais Dk. Mwinyi Mkoa wa Mjini Magharibi ni mwendelezo wa ziara zake za kukagua miradi ya maendeleo ikiwa ni shamrashamra za kusherekea mafaniko ya miaka mitatu ya uongozi wa awamu ya nane ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

alternative alternative alternative
Habari Nyingine

Nukuu za Viongozi