Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
WATANZANIA WANA IMANI KUBWA NA CCM, NI WAJIBU WA KILA KIONGOZI KUSHUGHULIKA NA KUTATUA KERO ZAO - KATIBU MKUU DKT. NCHIMBI
"CCM ni Chama cha kupigania haki ya wanyonge na lazima tuendeleze hilo katika kila ngazi kuanzia shina hadi taifa, wananchi wana imani kubwa na CCM hivyo ni wajibu wa kila kiongozi lazima tushughulikie kero na matatizo ya wananchi wetu."
"Katika miaka 3 serikali ya CCM chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imefanya mambo makubwa sana, msione haya kuyatangaza na kuyasemea, siasa ni lazima useme ulichofanya bila kusema hata aliyeshudia ukifanya atafanya kama hajaona, wengine watasema bana si wajibu wenu kufanya yani atachukulia kirahisi na bila kujali, lazima tuisemee vema serikali yetu inayowajali wananchi wake kwakuwa ni serikali inayojitambua"
"Tokeni vifua mbele kutetea serikali yenu"
"Mnaposimamia utekelezaji wa ilani msitafute maslahi binafsi, acheni kuwafata viongozi wa serikali kuomba hela kwa kuwatisha na kuweka uongo ndani yake, tunajua wapo viongozi wa CCM wa namna hiyo sasa hiyo si haki bali ni ukandamizaji na wizi, tutumie wajibu wetu wa haki kama wana CCM"
"Kero ya umeme tunakwenda kuitatua kwa kasi hapa Katavi, tumemsikia Mwenezi amelieleza vema hilo"
🗓️ 13 Aprili, 2024
📍Mpanda - Katavi
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.