SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA KIPAOMBELE KWENYE KUKUZA UCHUMI WAKE NA KUONGEZA UWEKEZAJI WA HUDUMA ZA JAMII IKIWEMO AFYA, ELIMU, NA HUDUMA NYINGINE ZA JAMII KAMA KUIMARISHA UMEME NA MAJI SAFI VIJIJINI.
SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema imeweka kipaumbele kwenye kukuza uchumi wake na kuongeza uwekezaji wa huduma za jamii ikiwemo afya, elimu, afya na huduma nyingine za jamii ikiwemo kuimarisha umeme na maji safi vijijini.
Aidha, imeeleza inavyojikita kwenye kilimo kinachozingatia zaidi hali ya hewa ili kuendana sambamba na nyakati za mavuno kwa lengo la kuwaletea tija Watanzania.
Akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutanao wa Kimataifa wa tathmini ya muda, kati ya mzunguko wa 20 wa Mapitio ya benki ya Dunia (IDA) kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, ukumbi wa Golden Tulip, Uwanja wa ndege, Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema, Tanzania inavyoshirikiana na Benki ya Dunia kwa kufanyakazi madhubuti ya kuwaondoa mamilioni ya watu kutoka kwenye umaskini na kuwaletea mabadiliko kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo inayofadhiliwa na benki hiyo.
Alisema, Tanzania imezindua mpango wa “Kujenga Kesho Bora” ambapo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesaidia wanawake na vijana wengi kupatiwa mafunzo, rasilimali ardhi kwa ajili ya kilimo cha kisasa, kuwawezesha kiuchumi, pembejeo na uongezaji thamani wa mazao ya kilimo na ufugaji katika kujitegemea wenyewe kiuchumi na kujikimu. “Tunashukuru Benki ya Dunia na washirika wengine kwa msaada wao kwa mpango huu”. Alishukuru Dk. Samia.
Rais Dk. Mwinyi alieleza, kwa msaada wa IDA wa dola za Marekani milioni 200 kwa Mpango wa Umeme Vijijini umeisaidia Tanzania kuwafikia zaidi ya watu milioni 2.5, hali iliyoisaidia nchi kufikia viwango vya upanuzi wa haraka barani Afrika kwa kipindi cha muongo mmoja uliopita. Alisema, zaidi ya watu milioni 4.5, wamefikiwa na huduma bora za jamii ikiwemo umeme vijijini, hospitali na ujenzi wa shule za vijijini.
Alisema mpango huo uliongeza fursa za ajira, biashara na matokeo bora kwa wanafunzi walioishi maeneo mbali na shule. Pia alisema, mpango ulikuwa na matokeo mazuri kiasi ya kuvutia ufadhili wa ziada wa dola za Marekani milioni 335 kusaidia kufikia matokeo bora zaidi kwa jamii za vijijini.
Akizungumzia sekta ya maji, chini ya miaka mitano ya mfuko wa msaada wa dola za Marekani milioni 300 kwa ajili ya Mpango Endelevu wa Ugavi wa Maji Vijijini na Usafi wa Mazingira uliwezesha upatikanaji wa maji safi kwa zaidi ya watu milioni 4.7, nusu yao wakiwa wanawake. Alieleza, mpango huo pia uliboresha upatikanaji wa huduma za vyoo kwa zaidi ya watu milioni 6.6, vituo vya afya 1,904 na skuli za msingi 1,095.
Pia, Rais Dk. Mwinyi alizungumzia mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya Tabianchi (COP28) uliofanyika Dubai ambako Rais Dk. Samia alitetea ajenda ya kusaidia kupunguza nishati mimea zinazoathiri mazingira mara baada ya kuongoza uzinduzi wa mradiri wa nishati safi ya kupikia itakayowanufaisha wanawake wengi, Afrika (AWCCSP). Akizungumzia Zanzibar inavyonufaika na fursa kutoka Benki ya Dunia, Rais Dk. Mwinyi alieleza uchumi wa Zanzibar unategemea Utalii kwa kiasi kikubwa hasa utalii wa utamaduni. Alisema, hifadhi ya Mji Mkongwe ambao ni urithi wa Dunia wa UNESCO, ulinufaika na Benki ya Dunia kupitia mradi wa “huduma za Mijini, Zanzibar” (ZUSP) ambao ulipata msaada kutoka IDA wenye thamani ya dola za Marekani milioni 93 ili kuboresha upatikanaji wa huduma za mijini na kuhifadhi urithi huo wa kitamaduni.
Alieleza pia mradi huo ulikarabati kipande cha mita 340 cha ukuta wa bahari ya Mizingani uliokuwa hatarini kuporomoka na kuzorotesha usafiri wa kivuko kwa wafanyabiashara na watalii. Sambamba na kuboresha barabara kuu ya Mji Mkongwe. Alieleza Benki ya Dunia pia imesaidia Tanzania kupitia Mitandao ya Hifadhi ya Jamii ambayo ilitolewa kwa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) na Mradi wa Ushirikiano wa Usafiri kwa ajili ya kuboresha barabara. Alisema, ushirikiano mwema uliopo baina ya Tanzania na Benki ya Dunia umesaidia maisha ya mamilioni ya watu nchini nakuongeza kuwa ushirikiano huo utaendelea kudumu.
Rais, Dk. Mwinyi aliiomba Benki ya Dunia na washirika wake, kuendelea kuimarisha usaidizi wao kwa nchi wanufaika wa IDA ili kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs). Pia Dk. Mwinyi aligusia eneo la biashara huria kwa mataifa wanufaika wa Benki ya Dunia na washirika wake, ili kuimarisha ushindani na uundaji wa nafasi za kazi kupitia ushirikiano wa kikanda na biashara, kwa bara la Afika na maeneo mengine ya dunia, “Tunaamini IDA na IFC zinahitaji kuongeza usaidizi ili kukuza sekta binafsi inayostawi, jambo la msingi ni kuunganisha biashara za Kiafrika katika minyororo ya thamani ya kimataifa na kuvutia FDIs.” Alieleza Rais Dk. Mwinyi.
Akizungumza kwenye mkutano huo, Rais wa Benki ya Dunia na washirika wake, Ajei Banga alimpa pole Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan kwa mtihani wa majanga ya kimaumbile yaliyowakumba Watanzania wa Manyara, nakueleza kuwa Benki ya Dunia ilipokea taarifa kwa masikitiko makubwa. Mapema akizungumza kwenye mkutano huo waziri wa Fedha wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Lameck Nchemba aliiomba Benki ya Dunia kuwaongeza watanzania wa Mkoa wa
Manyara walioathiriwa na mafuriko hivi karibuni kupitia fao la benki hiyo la majanga ya kimaumbile.
Naye, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Dk. Saada Mkuya Salum, alieleza mafanikio makubwa ya mkutano huo wa Kimataifa wa tathmini ya muda, kati ya mzunguko wa 20 wa Mapitio ya benki ya Dunia (IDA) yamefikiwa kutokana na jukudi kubwa za uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa ushirikiano wa karibu na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na msaada mkubwa waliopata kutoka kwa Mwakilishi Mkaazi wa benki hiyo, Bw. Nathan Balete.
Zaidi ya wageni 300 kutoka mataifa mbalimbali dunia wamehudhuria mkutano huo wenye lengo la kufanya mapitio ya miradi inayoungwa mkono na benki hiyo, pamoja na mambo mengine pia utaangalia namna bora ya utekelezwaji wa miradi ya maendeleo na namna ya kuongezwa fedha na ruzuku kwa miradi itakayofanya vizuri zaidi kwa mataifa wanufaika.
𝐒𝐀𝐒𝐀 𝐍𝐈 𝐙𝐀𝐌𝐔 𝐘𝐀 𝐏𝐖𝐀𝐍𝐈; 𝐀𝐑𝐃𝐇𝐈 𝐘𝐀 𝐇𝐈𝐒𝐓𝐎𝐑𝐈𝐀, 𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐀𝐍𝐀𝐊𝐔𝐉𝐀!!!!!
27-06-2026
𝐈𝐑𝐈𝐍𝐆𝐀 𝐌𝐉𝐈𝐍𝐈 𝐘𝐀𝐌𝐏𝐀 𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐌𝐀𝐏𝐎𝐊𝐄𝐙𝐈 𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐇𝐈𝐒𝐓𝐎𝐑𝐈𝐀
27-06-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐀𝐙𝐈𝐍𝐃𝐔𝐀 𝐒𝐇𝐈𝐍𝐀 𝐋𝐀 𝐖𝐀𝐊𝐄𝐑𝐄𝐊𝐄𝐓𝐖𝐀 𝐌𝐋𝐀𝐍𝐃𝐄𝐆𝐄, 𝐊𝐈𝐋𝐎𝐒𝐀-𝐈𝐑𝐈𝐍𝐆𝐀
27-06-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐀𝐓𝐄𝐌𝐁𝐄𝐋𝐄𝐀 𝐒𝐇𝐈𝐍𝐀 𝐍𝐀. 𝟏𝟎 𝐌𝐀𝐅𝐈𝐅𝐈, 𝐀𝐒𝐈𝐒𝐈𝐓𝐈𝐙𝐀 𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈, 𝐔𝐌𝐎𝐉𝐀 𝐍𝐀 𝐌𝐒𝐇𝐈𝐊𝐀𝐌𝐀𝐍𝐎
27-06-2026
𝐌𝐑𝐀𝐃𝐈 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐎 𝐘𝐀 𝐔𝐅𝐔𝐍𝐃𝐈 𝐊𝐈𝐋𝐎𝐋𝐎 𝐊𝐔𝐅𝐔𝐍𝐆𝐔𝐀 𝐅𝐔𝐑𝐒𝐀 𝐙𝐀 𝐀𝐉𝐈𝐑𝐀 𝐊𝐖𝐀 𝐕𝐈𝐉𝐀𝐍𝐀
27-06-2026
𝐊𝐈𝐋𝐎𝐋𝐎, 𝐙𝐀𝐌𝐔 𝐘𝐄𝐍𝐔 𝐍𝐈 𝐋𝐄𝐎!
27-06-2026
𝐑𝐀𝐁𝐈𝐀: 𝐃𝐊𝐓. 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐒𝐔𝐋𝐔𝐇𝐔 𝐇𝐀𝐒𝐒𝐀𝐍 𝐍𝐈 𝐌𝐓𝐄𝐊𝐄𝐋𝐄𝐙𝐀𝐉𝐈 𝐌𝐀𝐇𝐈𝐑𝐈 𝐖𝐀 𝐀𝐇𝐀𝐃𝐈 𝐙𝐀 𝐂𝐂𝐌
27-06-2026
𝐒𝐈𝐌𝐔 𝐈𝐌𝐄𝐈𝐓𝐀, 𝐍𝐄𝐄𝐌𝐀 𝐘𝐀 𝐔𝐓𝐀𝐓𝐔𝐙𝐈 𝐊𝐈𝐋𝐎𝐋𝐎!
27-06-2026
𝐑𝐔𝐀𝐇𝐀 𝐌𝐁𝐔𝐘𝐔𝐍𝐈 𝐘𝐀𝐅𝐔𝐑𝐈𝐊𝐀; “𝐂𝐇𝐈𝐄𝐅 𝐂𝐇𝐎𝐆𝐀𝐕𝐀𝐓𝐀𝐌𝐁𝐔𝐋𝐄” 𝐀𝐊𝐈𝐓𝐄𝐊𝐀 𝐌𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐎 𝐖𝐀 𝐇𝐀𝐃𝐇𝐀𝐑𝐀!
27-06-2026
𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐎 𝐂𝐇𝐀 𝐔𝐌𝐖𝐀𝐆𝐈𝐋𝐈𝐀𝐉𝐈 𝐍𝐈 𝐔𝐅𝐔𝐍𝐆𝐔𝐎 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐏𝐈𝐍𝐃𝐔𝐙𝐈 𝐘𝐀 𝐔𝐂𝐇𝐔𝐌𝐈 𝐖𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈: 𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈
27-06-2026
𝐂𝐂𝐌 𝐘𝐀𝐔𝐍𝐆𝐀 𝐌𝐊𝐎𝐍𝐎 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈 𝐖𝐀 𝐍𝐉𝐎𝐌𝐁𝐄 𝐊𝐖𝐀 𝐊𝐀𝐙𝐈 𝐙𝐀 𝐔𝐙𝐀𝐋𝐈𝐒𝐇𝐀𝐉𝐈 𝐌𝐀𝐋𝐈
27-06-2026
𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐍𝐈 𝐌𝐒𝐈𝐍𝐆𝐈 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐄𝐍𝐃𝐄𝐋𝐄𝐎: 𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈
27-06-2026
𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈 𝐑𝐀𝐒𝐌𝐈 𝐈𝐑𝐈𝐍𝐆𝐀!!
27-06-2026
𝐑𝐀𝐁𝐈𝐀 𝐀𝐏𝐎𝐊𝐄𝐋𝐄𝐖𝐀 𝐍𝐉𝐎𝐌𝐁𝐄, 𝐀𝐇𝐈𝐌𝐈𝐙𝐀 𝐕𝐈𝐎𝐍𝐆𝐎𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐊𝐔𝐈𝐒𝐇𝐈 𝐃𝐇𝐀𝐍𝐀 𝐘𝐀 𝐊𝐀𝐙𝐈 𝐍𝐀 𝐔𝐓𝐔 𝐊𝐖𝐀 𝐕𝐈𝐓𝐄𝐍𝐃𝐎
27-06-2026
𝐑𝐀𝐁𝐈𝐀: 𝐂𝐂𝐌 𝐇𝐀𝐈𝐓𝐀𝐕𝐔𝐌𝐈𝐋𝐈𝐀 𝐔𝐙𝐄𝐌𝐁𝐄, 𝐕𝐈𝐎𝐍𝐆𝐎𝐙𝐈 𝐖𝐀𝐖𝐀𝐉𝐈𝐁𝐈𝐊𝐄 𝐊𝐔𝐓𝐀𝐓𝐔𝐀 𝐂𝐇𝐀𝐍𝐆𝐀𝐌𝐎𝐓𝐎 𝐙𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈
27-06-2026
𝐈𝐑𝐈𝐍𝐆𝐀 𝐓𝐔𝐍𝐀𝐊𝐔𝐉𝐀𝐀𝐀, 𝐓𝐔𝐍𝐀𝐀𝐍𝐙𝐈𝐀 𝐑𝐔𝐀𝐇𝐀 𝐌𝐁𝐔𝐘𝐔𝐍𝐈!
27-06-2026
𝐌𝐈𝐊𝐎𝐏𝐎 𝐘𝐀 𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈𝐌𝐈𝐀 𝟏𝟎% 𝐘𝐀𝐂𝐇𝐎𝐂𝐇𝐄𝐀 𝐔𝐂𝐇𝐔𝐌𝐈 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐊𝐔𝐍𝐃𝐈 𝐌𝐀𝐀𝐋𝐔𝐌
27-06-2026
𝐍𝐃𝐆 𝐑𝐀𝐁𝐈𝐀 𝐀𝐏𝐎𝐊𝐄𝐋𝐄𝐖𝐀 𝐑𝐔𝐕𝐔𝐌𝐀, 𝐀𝐇𝐈𝐌𝐈𝐙𝐀 𝐔𝐌𝐎𝐉𝐀 𝐍𝐀 𝐌𝐒𝐇𝐈𝐊𝐀𝐌𝐀𝐍𝐎 𝐍𝐃𝐈𝐎 𝐍𝐆𝐔𝐕𝐔 𝐘𝐀 𝐂𝐂𝐌
27-06-2026
𝐊𝐇𝐄𝐑𝐈 𝐘𝐀 𝐒𝐈𝐊𝐔 𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐌𝐀𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀 𝐘𝐀 𝐌𝐓𝐎𝐓𝐎 𝐖𝐀 𝐀𝐅𝐑𝐈𝐊𝐀
27-06-2026
𝐌𝐇𝐄. 𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐀𝐍𝐀𝐖𝐀𝐏𝐄𝐍𝐃𝐀 𝐒𝐀𝐍𝐀 𝐖𝐀𝐓𝐀𝐍𝐙𝐀𝐍𝐈𝐀, 𝐖𝐀𝐓𝐔𝐌𝐈𝐒𝐇𝐈 𝐖𝐀 𝐔𝐌𝐌𝐀 𝐓𝐈𝐌𝐈𝐙𝐄𝐍𝐈 𝐖𝐀𝐉𝐈𝐁𝐔 𝐖𝐄𝐍𝐔 𝐊𝐈𝐊𝐀𝐌𝐈𝐋𝐈𝐅𝐔: 𝐑𝐀𝐁𝐈𝐀
27-06-2026