MWENYEKITI WA UMOJA WA VIJANA WA CHAMA CHA MAPINDUZI (UVCCM) TAIFA, MOHAMED ALI MOHAMED (KAWAIDA), AWATAKA VIJANA KUWALINDA VIONGOZI WAO KWA VITENDO
MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Mohamed Ali Mohamed (Kawaida), amesema vijana wa Chama hicho haitoshi kulinda Viongozi wao kwa maneno badala yake wajielekeze katika vitendo vinavyobeba dhamira, mikakati na ujasiri wa kuleta ufanisi ndani ya Chama na Jumuiya zake.
Kauli hiyo ameitoa katika ufungaji wa mafunzo elekezi ya Viongozi wa UVCCM Mkoa wa Kusini Unguja,yaliyofanyika katika Chuo cha Mafunzo na Uongozi kilichopo Tunguu Zanzibar.
Alisema kuwa Vijana wa UVCCM wamatakiwa kuwa imara wakati wote kwani ndio wenye dhamana kubwa ya kulinda kwa gharama yoyote maslahi ya Chama na Jumuiya zake pamoja na Viongozi wake.
Katika maelezo yake Mwenyekiti huyo MCC Mohamed Kawaida, alisema historia inaonyesha kuwa Umoja huo ndio chimbuko la kuwaandaa Viongozi bora nchini walioiva kimaarifa,kiujuzi,kimaadili, uaminifu, wachapakazi na wenye uzalendo wa kweli.
"Haitoshi kusema, kuimba na kuwasifu tu Viongozi wetu badala yake tuonyeshe misimamo, dhamira, utetezi na ulinzi wetu kwa vitendo na hoja imara zinazoendana mahitaji ya siasa za Sasa. ", alisema Mwenyekiti huyo Mohamed Kawaida.
Mohamed, aliwasihi washiriki wa mafunzo hayo kutumia mbunu, maelekezo na nasaha walizopewa kuleta Mabadiliko chanya katika maeneo yao ya kiutendaji.
Pamoja na hayo alikwambia washiriki hao wa mafunzo kuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuwa ameendelea kufanya kazi kubwa ya kufungua milango ya uwekezaji inayotoa fursa za ajira kwa vijana wa rika na fani mbalimbali nchini.
Kupitia hafla hiyo aliwasihi Vijana mbalimbali nchini kujipanga vizuri ili waweze kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za Uongozi katika Uchaguzi Mkuu ujao wa Mwaka 2025.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar ambaye pia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja huo Mussa Haji Mussa, alipongeza washiriki wa mafunzo hayo kwa nidhamu na juhudi zao katika kufuatilia mada zilizotolewa katika mafunzo.
Akisoma risala Katibu wa UVCCM Mkoa wa Kusini Unguja Mohamed Ali Mohamed, alisema mafunzo hayo ya siku tatu ya kuwajengea uwezo vijana wa UVCCM Mkoa wa Kusini Unguja yamefanyika kwa ufanisi mkubwa.
Alisema katika mafunzo hayo zimetolewa mada mbalimbali zikiwemo Historia ya CCM na Jumuiya zake, muundo wa CCM na Jumuiya zake, mipaka na majukumu ya Viongozi wa CCM na Jumuiya zake, Historia ya Mapinduzi ya Zanzibar na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Kupitia risala hiyo wamewapongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi zake za kuimarisha Uchumi kupitia mradi wa uwekezaji katika Bandari Dar es salaam utakaotekelezwa na Kampuni ya DP World kutoka Dubai.
Jumla ya Vijana Jumla 207 wanaume 124 wanawake 83 wa UVCCM Mkoa wa Kusini Unguja wamehitimu mafunzo hayo elekezi na kutunukiwa vyeti
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
28-10-2025
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
28-10-2025
π¨ππππ£πππππ πͺπ πππ§. π¦ππ ππ π¨π ππππ§π ππ ππ‘π ππͺπ πͺππ£ππ‘πππ‘π, πͺππππ¨ππππ πππ
πππ©πππͺ ππ πͺπͺ πΏπ π©. πππππ§π€ ππ¬ππ₯π€π ππ πππ€π£ππ€π―π π¬π πΎππΌπΏπππΌ π£π πΌπΎπ
28-10-2025
πππ§. π¦ππ ππ ππ§π¨π π‘πππ‘π π¬π ππ₯πππ π¬π ππππ’π π
28-10-2025
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
28-10-2025
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
28-10-2025
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
28-10-2025
WANACHAMA 280 WA CHADEMA WATIMKIA CCM
28-10-2025
BALOZI NCHIMBI: MAONI YOYOTE KUHUSU AMANI YA TANZANIA HAYATAPUUZWA
28-10-2025
π¦ππ₯πππππ π¬π π₯πππ¦ πππ§. π¦ππ ππ ππ ππͺπππ ππππ π π¬π π πππ‘πππππ’ ππππ π¦ππππ π¨ - ππ£π. ππ π’π¦ π ππππππ
28-10-2025
MAKALLA: BARABARA YA MPWAPWA NJIAPANDA KONGWA KUJENGWA LAMI
28-10-2025
BALOZI NCHIMBI AWASILI ARUSHA
28-10-2025
TAARIFA KWA UMMA
28-10-2025
UCHAGUZI MKUU SIO AJALI-WASIRA
28-10-2025
πͺπππ¨π ππ π π¦ππππππ¨π π©ππ’π‘ππ’ππ ππππππππ ππͺππ‘π¬π ππ¨π₯π ππ π ππ’π‘π - (π ππ) πππ©π¨
28-10-2025
MONGELLA AONGOZA MAZISHI YA KADA WA CCM JIJINI MWANZA
28-10-2025
ASIYETII SHERIA, KATIBA NA KUWA TAYARI KUUA KWA MASLAHI BINAFSI HUO NI UGAIDI’
28-10-2025
πππ π¬ππ¦ππ¦ππ§πππ πͺπππ’π πππ ππ¨πππππππͺπ ππͺπ ππ¨πππ‘πππ§ππ π¨πͺπππ’, π¨πππππ‘ππ’ π‘π π¨πππππππ¨, π¬ππππ ππ π πππ¨π‘ππ - πππ. πππ©π¨
28-10-2025
KAENI KIMYA KAMA HAMJUI NCHI ILIKOTOKA - WASIRA
28-10-2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefungua kiwanda cha kutengeneza mabomba ya maji na uchakataji pamba cha MOLI Oil Mills Co. Ltd kilichopo Bariadi Mkoani Simiyu tarehe 16 Juni, 2025.
28-10-2025