Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
MKUTANO WA KATIBU MKUU NA WANANCHI WA HANANG MKOA WA MANYARA
Matukio mbalimbali katika picha Mkutano wa hadhara Hanang' Manyara, Katibu Mkuu Balozi Ndg. Dkt. Emmanuel Nchimbi akizungumza na wananchi.
Katibu Mkuu yupo katika ziara ya siku mbili mkoani Manyara kufuatilia Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020/25.Katibu Mkuu ameambatana na Katibu wa NEC-Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndg. Amos Makalla na Katibu wa NEC-Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg. Rabia Abdallah Hamid.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.