CCM YASHIRIKI TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024
CCM YASHIRIKI TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara Ndgu. John Mongella ameshiriki kwenye uzinduzi wa Tangazo la Uchaguzi wa Serikali za Mtaa Kwa niaba ya Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi huku mgeni rasmi wa uzinduzi huo akiwa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohammed Mchengerwa.
Mchengerwa amesema
"uchaguzi wa serikali za mitaa Tanzania Bara kwa mwaka 2024 utafanyika Novemba 27 na Upigaji wa kura utaanza
saa mbili kamili asubuhi na kumalizika saa kumi kamili jioni.
Waziri Mchengerwa ameyasema hayo leo Agosti 15,2024 Jijini Dodoma , wakati akitoa tangazo la uchaguzi wa serikali za Mitaa kwa mwaka 2024 lililoambatana na uzinduzi wa nembo itakayatumika kwenye uchaguzi pamoja na utolewaji wa muongozo wa uchaguzi huo"
"Nafasi zitakazogombewa katika uchaguzi huu
ni Mwenyekiti wa kijiji, wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji (kundi mchanganyiko la wanaume na wanawake), wajumbe wa Halmashauri
ya Kijiji (kundi la wanawake) na wenyeviti wa vitongoji katika Mamlaka
za Wilaya.Kwa nafasi hizo,uchaguzi utaendeshwa kwa mujibu wa
Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kijiji, Wajumbe wa Halmashauri
ya Kijiji na Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Wilaya za Mwaka
2024 (Tangazo la Serikali Na. 571 la Mwaka 2024), nyingine ni Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Miji Midogo. Kwa nafasi
hiyo, uchaguzi utaendeshwa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Miji Midogo za Mwaka
2024 (Tangazo la Serikali Na. 572 la Mwaka 2024),
Nakuongeza kuwa "nafasi nyingine ni Mwenyekiti wa kijiji, wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji (kundi
mchanganyiko la wanaume na wanawake), wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji (kundi la wanawake) na wenyeviti wa vitongoji katika Mamlaka
za Miji. Kwa nafasi hizo, uchaguzi utaendeshwa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kijiji, Wajumbe wa
Halmashauri ya Kijiji na Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za
Miji za Mwaka 2024 (Tangazo la Serikali Na.573 la Mwaka 2024) na Mwenyekiti wa mtaa na wajumbe wa kamati ya mtaa (Kundi
Mchanganyiko la Wanaume na Wanawake) na wajumbe wa kamati ya
mtaa (Kundi la Wanawake) katika Mamlaka za Miji. Kwa nafasi hizo,
uchaguzi utaendeshwa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa
Mwenyekiti wa Mtaa na Wajumbe wa Kamati ya Mtaa katika Mamlaka
za Miji za Mwaka 2024 (Tangazo la Serikali Na. 574 la Mwaka 2024), " ameeleza Mchengerwa
Aidha, katika hatua nyingine Mchengerwa amezitaka Taasisi zinazotaka kutoa elimu ya mpiga kura kufanya maombi maalumu kupitia kwa Katibu Mkuu wa ofisi ya Rais TAMISEMI ili wapate kibali cha kutoa elimu hiyo kwa kuzingatia miongozo iliyotolewa.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Ndg. Juma Ali Khatibu amesema wao kama Baraza la Vyama vya Siasa hawategemei kuona migogoro baada ya Uchaguzi kwani kuna maisha mengine yataendelea baada ya Uchaguzi.
Pia ametoa wito kwa watendaji wa TAMISEMI watakaohusika katika usimamizi wa mchakato wa uchaguzi huo kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa haki na weledi na kuzingatia Taaluma zao na misingi ya Haki ili kutimiza zile 4R za Rais Samia.
Naye Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa Martin Shigella amesema ushiriki wa Viongozi wa vyama vya siasa katika mchakato wa leo unakwenda kuongeza hari na hamasa kwa wananchi kushiriki katika uchaguzi huo.
"Hata sisi kule mikoani tuna viongozi wa vyama vya siasa na tunashirikiana nao Sana katika kuhakikisha uchaguzi huu una kuwa wa haki na uhuru ili kuhakikisha wanapatikana viongozi bora ambao watatanguliza maslahi ya Taifa mbele," ameeleza Shigella
Kampeni za UCHAGUZI wa serikali za mitaa 2024 zitafanyika siku saba
kabla ya siku ya uchaguzi. Aidha, Kanuni zinaelekeza, kila Chama cha
Siasa kinachoshiriki uchaguzi kitawasilisha ratiba yake ya mikutano ya
kampeni ya uchaguzi kwa Msimamizi wa Uchaguzi si chini ya siku saba
kabla ya kuanza kwa kampeni.
KIPINDI MAALUMU
09-06-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐀𝐒𝐈𝐌𝐀𝐌𝐈𝐒𝐇𝐀 𝐌𝐒𝐀𝐅𝐀𝐑𝐀 𝐊𝐔𝐒𝐀𝐋𝐈𝐌𝐈𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈 𝐍𝐀 𝐊𝐈𝐉𝐈𝐖𝐄 𝐂𝐇𝐀 𝐂𝐇𝐀𝐃𝐄𝐌𝐀 𝐀𝐑𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐌𝐉𝐈𝐍𝐈
09-06-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐀𝐓𝐄𝐌𝐁𝐄𝐋𝐄𝐀 𝐊𝐈𝐓𝐔𝐎 𝐂𝐇𝐀 𝐀𝐅𝐘𝐀 𝐊𝐀𝐋𝐎𝐋𝐄𝐍𝐈, 𝐀𝐑𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐌𝐉𝐈𝐍𝐈
09-06-2026
𝐀𝐑𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐘𝐀𝐀𝐌𝐁𝐈𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐂𝐇𝐀𝐆𝐔𝐀 𝐌𝐀𝐄𝐍𝐃𝐄𝐋𝐄𝐎 𝐁𝐀𝐃𝐀𝐋𝐀 𝐘𝐀 𝐌𝐀𝐀𝐍𝐃𝐀𝐌𝐀𝐍𝐎
09-06-2026
𝐌𝐀𝐏𝐎𝐊𝐄𝐙𝐈 𝐘𝐀 𝐊𝐀𝐓𝐈𝐁𝐔 𝐖𝐀 𝐍𝐄𝐂, 𝐈𝐓𝐈𝐊𝐀𝐃𝐈, 𝐔𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐍𝐀 𝐌𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐎 𝐂𝐂𝐌, 𝐍𝐃𝐔𝐆𝐔 𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐋𝐀𝐁𝐀𝐍 𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈, 𝐎𝐅𝐈𝐒𝐈 𝐙𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐖𝐈𝐋𝐀𝐘𝐀 𝐘𝐀 𝐀𝐑𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐌𝐉𝐈𝐍𝐈
09-06-2026
𝐒𝐀𝐒𝐀 𝐍𝐈 𝐀𝐑𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐌𝐉𝐈𝐍𝐈, 𝐌𝐖𝐄𝐍𝐃𝐎 𝐌𝐃𝐔𝐍𝐃𝐎!
09-06-2026
𝐀𝐑𝐔𝐌𝐄𝐑𝐔 𝐘𝐀𝐒𝐈𝐊𝐈𝐀 𝐖𝐈𝐓𝐎 𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐋𝐈𝐍𝐃𝐀 𝐌𝐀𝐀𝐃𝐈𝐋𝐈 𝐍𝐀 𝐇𝐀𝐊𝐈 𝐙𝐀 𝐖𝐀𝐓𝐎𝐓𝐎
09-06-2026
𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐀𝐒𝐀𝐌𝐁𝐀𝐙𝐀 𝐔𝐏𝐄𝐍𝐃𝐎 𝐖𝐀 𝐀𝐆𝐀𝐏𝐄 𝐊𝐖𝐄𝐍𝐘𝐄 𝐊𝐈𝐉𝐈𝐖𝐄 𝐂𝐇𝐀 𝐂𝐇𝐀𝐃𝐄𝐌𝐀 𝐀𝐑𝐔𝐌𝐄𝐑𝐔
09-06-2026
𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈 𝐀𝐀𝐍𝐙𝐀 𝐙𝐈𝐀𝐑𝐀 𝐀𝐑𝐔𝐌𝐄𝐑𝐔 𝐊𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐊𝐀𝐆𝐔𝐀 𝐔𝐇𝐀𝐈 𝐖𝐀 𝐂𝐇𝐀𝐌𝐀
09-06-2026
𝐌𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐎 𝐖𝐀 𝐇𝐀𝐃𝐇𝐀𝐑𝐀 𝐖𝐀 𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀 𝐖𝐈𝐋𝐀𝐘𝐀 𝐘𝐀 𝐊𝐀𝐑𝐀𝐓𝐔 - 𝐌𝐊𝐎𝐀 𝐖𝐀 𝐀𝐑𝐔𝐒𝐇𝐀
09-06-2026
𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐓𝐔𝐍𝐔𝐊𝐈𝐖𝐀 𝐒𝐇𝐀𝐇𝐀𝐃𝐀 𝐘𝐀 𝐇𝐄𝐒𝐇𝐈𝐌𝐀 𝐔𝐑𝐔𝐒𝐈
09-06-2026
𝐀𝐑𝐔𝐌𝐄𝐑𝐔, 𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐀𝐍𝐀𝐊𝐔𝐉𝐀!
09-06-2026
𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐑𝐀𝐒𝐌𝐈 𝐔𝐑𝐔𝐒𝐈, 𝐀𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐀 𝐍𝐀 𝐏𝐔𝐓𝐈𝐍
09-06-2026
𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎, 𝐓𝐔𝐍𝐀𝐊𝐔𝐉𝐀
09-06-2026
𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐃𝐊𝐓. 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐖𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈 𝐌𝐎𝐒𝐂𝐎𝐖, 𝐔𝐑𝐔𝐒𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐙𝐈𝐀𝐑𝐀 𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀
09-06-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀 𝐀𝐖𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈 𝐖𝐈𝐋𝐀𝐘𝐀 𝐘𝐀 𝐒𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐈𝐑𝐎 𝐊𝐖𝐀 𝐙𝐈𝐀𝐑𝐀 𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐊𝐀𝐙𝐈
09-06-2026
𝐅𝐔𝐍𝐆𝐀 𝐊𝐀𝐙𝐈 𝐌𝐊𝐎𝐀 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐍𝐘𝐀𝐑𝐀 𝐋𝐄𝐎!!!
09-06-2026
𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈 𝐀𝐓𝐄𝐌𝐁𝐄𝐋𝐄𝐀 𝐒𝐇𝐈𝐍𝐀 𝐍𝐀. 𝟐 𝐊𝐀𝐓𝐀 𝐘𝐀 𝐁𝐎𝐍𝐆𝐀
09-06-2026
𝐁𝐀𝐁𝐀𝐓𝐈 𝐌𝐉𝐈𝐍𝐈 𝐋𝐄𝐎 𝐓𝐔𝐍𝐀𝐈𝐅𝐔𝐍𝐈𝐊𝐀!!!
09-06-2026
𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈 𝐀𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐀 𝐍𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈 𝐇𝐀𝐍𝐀𝐍𝐆, 𝐀𝐒𝐈𝐊𝐈𝐋𝐈𝐙𝐀 𝐍𝐀 𝐊𝐔𝐓𝐀𝐓𝐔𝐀 𝐊𝐄𝐑𝐎 𝐙𝐀𝐎
09-06-2026