Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
ACHENI KUPANGA SAFU YA WENYEVITI KWA KUWAOGOPA MADIWANI NA WABUNGE - NDG. ISSA GAVU
> Akemea utoaji na upokeaji wa rushwa
"...Tukinyamaza kimya bila kusema kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya CCM maana yake tunaungana na wachache wasiokitakia mema chama chetu na kupotosha kwa lengo la kukichafua na serikali tunayoiongoza, lazima tukitendee chama chetu haki, wananchi na Rais wetu Mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan"
"Naamini sote tunajua nini maana ya wajibu wa dhima ya kiongozi wa chama na serikali."
"Ili tupate mtaji mzuri wa kushinda chaguzi za mwaka huu 2024 na mwakani 2025 lazima tubadilike, kwakuwa uhai wa CCM ni kuhakikisha kila mmoja wetu ana wajibu wa kuhamaisha CCM , lazima tuongeze idadi ya wanachama kwakuwa huo ndio mtaji wa kura."
"Uchaguzi wetu ni wa kidemokrasia na demokrsia ni kura zinapigwa na wanadamu lazima tuwe na idadi kubwa ya wanachama, wafuasi, na mashabiki na wakati wa kuboresha daftari la wapiga kura watu hao waende kwa wingi."
"Acheni kupanga safu ya wenyeviti na vitongoji, mkipanga safu kwa kuwaogopa madiwani na wabunge hamkitendei haki chama chetu, hatuhitaji ushindi unaotokana na makandokando , hatuna sababu ya kuendekeza rushwa wala kuendekeza wachache wasiotaka maslahi ya watu wengi, lazima jamii iendelee kutuamini kama kweli mategemeo ya kila mtanzania yapo ndani ya CCM."
Ndugu. Issa Haji Gavu
Katibu wa NEC - Oganaizesheni
Ameyasema hayo kwenye Mkutano wa kueleza muelekeo wa Chama pamoja na mambo mengine kuhusu uelekeo wa uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka huu wa 2024 na uchaguzi mkuu wa mwaka 2024.
Mkutano huu umekutanisha, Wajumbe wa Mashina na Wenyeviti wa Mitaa, Vijiji na Vitongoji na Miitaa, Viongozi wa Chama ngazi zote, Wazee mashuhuri, Viongozi wa Dini pamoja na Watendaji wa serikali ngazi zote na Taasisi zisizo za kiserikali.
🗓️ 13 Aprili, 2024
📍Mpanda - Mkoani Katavi
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.