Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


CCM NDIYO YENYE MKATABA NA WANANCHI KATIKA KUISIMAMIA SERIKALI - BALOZI DKT. NCHIMBI

alternative

> Awataka viongozi wa serikali kutambua kuwa CCM ndiyo yenye dhamana ya kuisimamia na kuiendesha serikali 

> Atoa pongezi kwa ushirikiano mzuri wa chama na serikali mkoani Mbeya 

> Awashukuru na kuwapongeza wananchi wa jimbo la Mbeya mjini kwa kuendelea kuwa na imani na Dkt. Tulia Ackson kwakuwa ameliheshimisha Taifa 

Katibu Mkuu wa Chama Chama Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi , amesema chama chochote cha siasa kinapokwenda kwenye uchaguzi ni lazima kipeleke ilani yake kwa wananchi na wananchi wakiikubali na kukichagua maana yake wanakipa dhamana na unakuwa mkataba wa kuiendesha na kuisimamia serikali kuhakikisha ilani ile inatekelezwa.

Balozi Dkt. Nchimbi amesema bahati mbaya kuna wakati mwingine unakuta baadhi ya maeneo kuna viongozi wa serikali wanashindwa kutambua kwamba CCM ndiyo yenye mkataba na wananchi wa kuiendesha serikali hivyo amewataka viongozi kutambua hilo na kuwa ni wana wajibu wa kuitekeleza ilani ya CCM kwa kishindo na kwa wakati.

Kulingana na hilo, Balozi Dkt. Nchimbi ametoa pongezi kwa Uongozi wa CCM na Serikali katika Mkoa wa Mbeya kwakuwa na ushirikiano mzuri hali iliyopelekea kutekelezwa kwa miradi mingi ya maendeleo pamoja na kuwahudumia wananchi ipasavyo.

" Tunapokwenda kwenye uchaguzi, chama chochote cha saisa kinakuwa kinapeleka ilani yake na ndivyo CCM tulivyofanya na wananchi wakatuchagua maana yake CCM ndiyo yenye mkataba wa kuisimamia na kuiendesha serikali...bahati mbaya wakati mwingine unakuta kuna maeneo viongozi wa serikali wanashindwa kutambua kwamba CCM ina mkatana na wananchi wa kuiendesha serikali, hapa Mbeya hongereni sana kwa kutambua hilo kwakuwa mmekuwa na ushirikiano mzuri kati ya Viongozi wa Chama na Serikali "

Pia, Balozi Dkt. Nchimbi ametoa pongezi kwa viongozi wa CCM mkoa wa Mbeya kwa usimamizi madhubuti wa utekelezaji wa ilani kwakuwa maeneo mengi yamevuka hadi asilimia 100%.

Aidha, Balozi Dkt. Nchimbi ametoa zawadi ya Tsh Milioni 2 kwa vijana wa hamasa mkoa wa mbeya kwa kufanya kazi kubwa ya kuendelea kuhamasisha watanzania kukiamini na kukipenda chama cha mapinduzi lakini kwa kuwa na maneno ya vionjo yaliyobeba jumbe zenye kueleza utekelezaji wa ilani.

🗓️17 Aprili, 2024
📍Jijini Mbeya

alternative alternative alternative
Habari Nyingine

Nukuu za Viongozi