Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


NDG. ISSA GAVU ASISITIZA FOMU YA URAIS MWAKANI 2025 NI MOJA NA NI YA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN

alternative

Katibu wa NEC - Oganaizesheni wa CCM Taifa, Ndugu. Issa Haji Gavu akizungumza na maelfu ya Wananchi waliojitokeza kwa wingi katika Mkutano wa hadhara unaoongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu. Balozi. Dkt. Emmanuel Nchimbi ikiwa ni kuanza kwa ziara yake ya Mikoa 6.

Ndugu. Gavu amesema kuwa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 katika fomu ya Urais wana CCM kwa pamoja wameridhia itakuwa moja pekee kwa Mwenyekiti wa CCM na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Aidha, Ndugu. Gavu ameendelea kusisitiza juu ya ushiriki wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji ambapo amewataka Viongozi kuendelea kuongeza idadi kubwa ya Wananchama hai wa CCM.

🗓️ 13 Aprili, 2024
📍 Mpanda - Katavi

alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine

Nukuu za Viongozi