Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR IMELISHUKURU SHIRIKA LA MAENDELEO LAUMOJA WA MATAIFA (UNDP) KWA JITIHADA ZAKE ZA KUENDELEA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI KUPITIA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema UNDP limekua msaada mkubwa kwa SMZ hasa kwa kuendelea kushirikiana kwenye masuala mbalimbali ya maendeleo ikiwemo kuiongezea nguvu na kuiwezesha kifedha Taasisi ya Ufuatiliaji na Usimamizi Utendaji Kazi Serikalini (PDB), Zanzibar ili kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
Dk. Mwinyi amesema hayo Ikulu, Zanzibar alipozungumza na Mwakilishi Mkaazi wa Shirika hilo, nchini Shigeki Komatsubara aliefika kumtembelea. Alisema, SMZ na UNDP zimekua na ushirikiano wa karibu kwa miaka mingi na wamekua wakiungamkono Serikali kwenye masuala mbalimbali ya maendeleo.
Rais Dk. Mwinyi alimueleza mgeni wake huyo, Sera kuu ya Uchumi wa Zanzibar ni Uchumi wa Buluu, hivyo alimueleza kuangalia fursa zaidi za kuungamkono eneo hilo pamoja na Sekta ya Utalii. Dk. Mwinyi pia alilipongeza Shirika la UNDP kwa juhudi zake za kusaidia vyombo vya Sheria nchini ikiwemo Bunge kwa Tanzania Bara, Baraza la Wawakilishi na Mahakama kwa kuzijengea uwezo taasisi hizo.
Naye, Bw. Shigeki Komatsubara, alimuahidi Rais Dk. Mwinyi kwamba UNDP itaendeleza Ushirikiano kwa kuendelea kufanyakazi pamoja na SMZ kupitia Sekta ya Uchumi wa Buluu pamoja na kuendelea kuiungamkono PDB kupitia miradi mbalimbali ya Serikali.
Akizungumza baada ya hafla hiyo, Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Ufuatiliaji na Usimamizi Utendaji Kazi Serikalini (PDB) Zanzibar, Dk. Josephine Rogate Kimaro alilishukuru Shirika la UNDP kwa ushirikiano mkubwa wanaoipatia PDB ikiwemo kuwajengea uwezo kwenye utendajikazi wao.
Alisema, UNDP limekua likiungamkono masuala mbalimbali ya maaendeleo ya taasisi hiyo hasa kwenye usimamizi na utekelezaji wa miradi ya kimkakati na kuweka mifumo ya utekeleza wa miradi ya vipaombele pamoja na kuisaidia taasisi hiyo kwenye ushajihishaji wa rasilimali zake.
Shirika la UNDP linatekeleza miradi sita barani Afrika, ikiwemo mitatu kwa Tanzania ambapo Zanzibar wanashirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kutekeleza miradi ya kupambana na matukio ya Uhalifu Zanzibar kwa
kusirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka chini ya ufadhili wa Serikali ya Uingereza na Umoja wa Ulaya (EU).
Mradi mwengine unaotekelezwa na UNDP ni uwezeshaji kwenye masuala ya utawala wa kisheria ambapo mradi unaangazia juu ya haki na wajibu kwenye masuala ya jinsia ikiwemo masuala ya wanawake na watoto.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.