Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUK) CCM Zanzibar Khadija Salum Ali,amesema Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kuthamini  uhusiano wa kisiasa na kijamii uliopo baina yake na  Chama Tawala cha Msumbiji cha Frelimo.

alternative

Hayo ameyasema wakati akizungumza na Balozi Mdogo wa Msumbiji anayefanyia kazi zake Zanzibar Agostinho Abacar Trinza,  huko Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.

Ndugu Khadija,alisema uhusiano huo ulianza kabla ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964  ambapo Tanzania kwa kiasi kikubwa ilisaidia Msumbiji kufanikisha malengo yake ya kujitawala yenye,hatua ambayo ni kumbukumbu muhimu katika historia ya ukomboni wa nchi za Bara la Afrika.

"Chama Cha Mapinduzi kinaheshimu na kulinda mahusiano yake na Vyama rafiki vyote duniani,lakini kwa upande wa Msumbiji urafiki wetu umekuwa wa kipekee kutokana na ukaribu wetu ambao kwa sasa wapo Wazanzibar na Watanzania wengi wanaishi Msumbiji na pia wapo Wananchi wengi wa Msumbiji waishi kwa amani hapa Zanzibar.",alisema Katibu huyo wa Kamati Maalum ya NEC Khadija.

Kwa upande wa Balozi mdogo wa Msumbiji Zanzibar  Agostinho Abacar Trinza,alisema Chama Frelimo na Serikali ya Msumbiji vinajivunia uwepo uhusiano wa kijamii unaotoa fursa kwa Wananchi wa Msumbiji kuishi kwa amani na utulivu nchini.

Balozi Trinza,aliwapongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Mwinyi kwa kazi kubwa ya kuwaletea Wananchi maendeleo endelevu katika nyanja za kiuchumi,kisiasa,kijamii na kidiplomasia.

"Tunaona namna Tanzania bara na Zanzibar zinavyopiga hatua kubwa ya maendeleo yote hayo yanafanyika kwa ufanisi,kutokana na uwepo wa amani na utulivu katika nchi hii",alieleza Balozi Trinza.

Baada ya mazungumzo hayo Balozi Agostinho Abacar,alitembelea maeneo mbali mbali ya kihistoria yaliyopo Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui pamoja na kuzuru kaburi la aliyekuwa Rais wa kwanza wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi marehemu Abeid Amani Karume

alternative alternative alternative
Habari Nyingine

Nukuu za Viongozi