Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


MBEYA IMEBEBA HISTORIA MUHIMU YA UKOMBOZI AFRIKA - WASIRA

alternative

Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara,  Stephen Wasira amewaeleza vijana mkoani Mbeya kuwa mkoa huo una historia kubwa katika ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika, hivyo ni jukumu lao kuilinda.

Wasira amesema hayo leo alipokuwa akipokewa rasmi mkoani humo katika Ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya.

"Nataka niwaambie hapa mkoani Mbeya, Chama chetu ni Chama cha historia, sisi ni muungano wa vyama vilivyoikomboa Tanzania na Afrika kwa ujumla, sisi sio chama cha kawaida.

"Vijana ambao hawaelewi ni kwamba sisi ndio tuliosaidia kuikomboa Afrika. Hapa Mbeya ndipo alipopitia Nelson Mandela, hapa Mbeya ndipo alipopitia Sam Nujoma, na wote walipopita hapa kulikuwa na mzee wetu mwanzilishi wa Chama cha TANU alikuwa anaitwa Mwakangale na yeye ndiye aliewasindikiza kutoka hapa mmoja baada ya mwengine kwenda Dar es Salaam kwa Mwalimu Julius Nyerere..." amesema.

Amesema viongozi hao waliokuwa katika harakati za ukombozi wa nchi zao hatimaye walifanikiwa kuwaondoa wakoloni na kuwawezesha Waafrika kuwa huru.

alternative alternative alternative
Habari Nyingine