Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


RAIS DKT.MWINYI ASHUHUDIA KARAFUU ZA MAGENDO BANDARINI WETE.

alternative

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi ametembelea Bandari ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba katika ziara  ya kushtukiza na kushuhudia karafuu za magendo  tani 9.5 zenye thamani ya shilingi milioni 140 zilizotaka kusafirishwa kwa magendo na kukamatwa kwa ushirikiano wa Vyombo vya ulinzi na usalama Mkoa wa Kaskazini Pemba vikiwemo Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA) na Kikosi cha Kuzuia Magendo (KMKM) tarehe 04 Januari 2024 , Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Aidha Rais Dkt.Mwinyi ameleeza kuwa Serikali imeamua asilimia 80 ya mauzo  ya karafuu katika soko la Dunia kumpatia mkulima wa karafuu na 20 kwa shirika la biashara Zanzibar (ZSTC) kutumika katika uendeshaji.

Vilevile Rais Dkt.Mwinyi amesema karafuu iliyokuwa bora inatoka Zanzibar kwa kuitunza vizuri  na kuisafisha bei yake itaendelea kuimarika duniani. 

Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi amewasihi wananchi wasifanye magendo kwa maana watapata hasara kulingana na sheria za nchi, pia amesema Serikali itaendelea kuongeza bei ya karafuu.

alternative alternative alternative
Habari Nyingine

Nukuu za Viongozi