Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema inahitaji uwekezaji mkubwa katika sekta ya Maji na Umeme ili kuongeza ufanisi wa hali ya juu wa huduma ya uhakika kwenye sekta hizo.

alternative

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza na uongozi wa Kampuni ya “WAPCOS Limited” ya nchini India, uliofika Ikulu Zanzibar.

Dk. Mwinyi amesema hadi sasa Zanzibar inapokea megawati 110 za nishati ya umeme, ambao pia inapata msaada kutoka Tanzania Bara, hivyo alisema, Serikali inadhamira ya kuzalisha umeme wake mwenyewe na iko tayari kushirikiana na kampuni yoyote itakayokuwa tayari ili kuanza hatua za upembuzi yakinifu.

Pia, Rais Dk. Mwinyi amesema Zanzibar inahitaji utafiti wa kina wa uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa nishati hizo kwa kuangalia zaidi uwekezaji na huduma za uhakika.

Dk. Mwinyi ameikaribisha kampuni ya “WAPCOS Limited” endapo inavutika kufanya kazi na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inakaribishwa.

Alisema, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na ya India ni wadau wakubwa kwenye huduma za jamii na imekua ikishirikiana kwenye nyanja mablimbali za Maendeleo ikiwemo elimu.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya “WAPCOS Limited, Rajni Kant Agrawal amesema kampuni yao imejika zaidi na kutoa huduma za ushauri hasa kwenye nishari za umeme, maji na miundombini na kueleza kuwa wako tayari kusirikiana na Serikali kwenye uwekezaji wa sekta hizo.

Alisema, kwa Tanzania tayari kampuni hiyo inafanyakazi maeneo ya Dar es Salaam, Bagamoyo na maeneo mengine ya nchi ikiwemo Zanzibar.

Kampuni ya “WAPCOS Limited” yenye makao makuu yake mjini New Delhi, India ni watoa huduma za ushauri kwa nyanja za rasilimali maji, nishati na miundombinu. Ilizinduliwa rasmi June 26, mwaka 1969, mjini New Delhi.

Ni kampuni yenye miradi kadhaa kote India, Asia na Afrika, iko chini ya umiliki wa Serikali ya India kwa usimamizi wa Wizara ya Jal Shakti nchini humo.

alternative alternative alternative
Habari Nyingine

Nukuu za Viongozi