Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla ameendelea kuwashukuru waumini wa dini ya kiislamu na wazanzibari kwa ujumla kwa kuendelea kuiunga mkono Serikali ya Awamu ya Nane (8) katika kuwaletea maendeleo wananchi wote

alternative

Ameyasema hayo alipokuwa akiwasalimia Waumini wa Masjid AL- SWAFAA uliopo Kikwajuni GONGONI  mara baada ya kumalizika kwa  Ibada ya Sala ya Ijumaa.

Alhajj Hemed amewashukuru wananchi kwa kuwa wavumilivu katika kipindi chote cha utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo inayopita katika maeneo yao na kuwahakikishia kuwa Serikali ya Awamu ya Nane inayoongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dkt. HUSSEIN ALI MWINYI imejipanga kuhakikisha inatatua changamoto zote zinazowakabili wananchi wa maeneo yote ya Zanzibar Mijini na Vijijini.

Aidha amesema kuwa kwa kuzingatia mahitaji ya wananchi wa Zanzibar  Serikali imeamua kujenga miundombinu ya barabara za mijini na vijini sambamba na kuimarisha sekta ya elimu na Afya pamoja na nyenginezo kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi wake bila ya ubaguzi wa aina yoyote.

Sambamba na hayo Alhajj Hemed amewataka wananchi wa Zanzibar kuendelea kuitunza tunu iliopo nchini ya Amani na Utulivu ambayo ndio chachu ya maendeleo ya Taifa pamoja na kuiweka nchi katika mikono salama siku hadi siku.

Mapema akitoa Khutba katika Sala ya Ijumaa, Maalim SULTWAN NASSOR SIMBA amewataka waumini wa dini ya Kiislam na Wazanzibari kwa ujumla kujitahidi kuchuma chumo la haalali katika mali zao jambo ambalo litapelekea kuweza kujipanga katika kufanya ibada ya Hijja kwa fedha za halali na kupata fadhila kutoka kwa Allah (S.W)

Aidha amewataka waumini kuzitumia vyema neema walizonazo ikiwemo mali zao katika kufanya amali njema na kufanya ibada kwa wingi katika miezi mitukufu ukiwemo mwezi wa ZUL-QAADA (Mfungo Pili) pamoja na kuwaombea dua wale wote ambao wanajiandaa na kwenda kufanya ibada ya hijja kwa mwaka huu wa 1445 Hijjiria.

alternative alternative alternative
Habari Nyingine

Nukuu za Viongozi