Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewataka wananchi wa kiwani na vitongoji vyake kuendelea kuitunza miundombinu inayojengwa na Serikali ikiwemo miundombinu ya Skuli ili kufikia malengo ya Mapinduzi Matukufu ya mwaka 1964 ya kutoa elimu bure kwa wazanzibari katika mazingira yaliyo bora zaidi
Ameyasema hayo wakati akiweka Jiwe la Msingi katika Ujenzi wa Skuli ya Sekondari Kiwani Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba ikiwa ni muendelezo wa shamra shamra za kutimiza miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha inajenga skuli za ghorofa kila Wilaya na kila sehemu ambayo inachangamoto ya upatikanaji wa elimu sambmba na kuweka mazingira mazuri katika skuli hizo ikiwemo vifaa na rasilimali zinazohitajika ili kuongeza ufanisi katika usimamizi na ufuatiliaji wa maendeleo ya elimu katika skuli zote za Zanzibar.
Mhe. Hemed amesema kuwa Serikalini imekuwa ikitumia fedha nyingi katika kuboresha miundombinu ya elimu hivyo ni wajibu wa kila mwananchi kuhakikisha jengo la skuli hiyo pamoja na vifaa vyake wanavitunza vyema ili kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali ya kuwapatia elimu wananchi wake katika mazingira mazuri ikiwa ndio azma ya waasisi wa mapinduzi matukufu ya mwaka 1964.
Aidha amesema kuwa Skuli ya Sekondari Kiwani itakapokamilika itakuwa na kiwango cha hali ya juu na vifaa vya kisasa vya kusomea na kufundishia hivyo amewataka wazazi na walezi kuwasimamia vyema watoto wao katika kupata elimu ambayo itaweza kutoa wataalamu waliobora wenye kuisaidia nchi yao katika kuleta maendeleo.
Mhe. Makamo amewataka wananchi wa Kiwani kuyalinda na kuyaenzi Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na kutokuwa tayari kushawishiwa na watu wasioipendelea mema Zanzibar kwa kuyadharau na kuyabeza Mapinduzi ambayo ndio yaliyomkomboa mwananchi mnyonge wa Zanziabar.
Sambamba na hayo Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar amewataka wananchi wa kijiji cha kiwani na vijiji jirani kushikamana katika kuleta maendeleo jambo ambalo litakipatia sifa njema kijiji chao.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Lela Mohammed Mussa amesema katika jimbo la kiwani kuna jumla ya Skuli Nne (4) za ghorofa za kisasa ikiwemo Suli ya Sekondari ya Kiwani, hivyo amewataka walimu kuongeza bidii katika ufundishaji ili kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wa wilaaya ya Mkoani.
Waziri Lela amesema wilaya ya Mkoani ndio wilaya inayoongoza kwa Matokeo ya Darasa la saba (7) Zanzibar, hii imetokana na kuongezeka kwa maslahi ya walimu na ajira katika sekta ya Elimu ndiko kulikopelekea kuongezeka kwa ufaulu kwa wanafunzi wa Wilaya ya Mkoani na Zanzibar kwa ujumla.
Akisoma Taarifa ya kitaalamu juu ya ujenzi wa mradi wa Skuli ya Kiwani Sekondari, Katibu Mkuu Mkuu Wizara ya elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ndugu Khamis Abdalla amesema kukamilika kwa ujenzi wa skuli hiyo kutatoa nafasi kwa wanafunzi kuingia skuli kwa mkondo mmoja tu wa asubuhi na kupunguza msongamano wa wanafunzi madarasani.
Ndugu Khamis amefahamisha kuwa ujenzi huo wa Skuli ya gorofa tatu (3) hadi kumalizika kwake itagharimu shilingi za Kitanzania Bilioni 6.2 ambayo ni skuli kubwa kwa Zanzibar nzima iliyo na madarasa zaidi ya 45 itakayokidhi mahitaji yote anayotakiwa kupatiwa mwanafunzi ili kufikia malengo yao.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.