𝗖𝗗𝗘. 𝗚𝗔𝗩𝗨 𝗔𝗖𝗛𝗔𝗥𝗨𝗞𝗔, 𝗔𝗦𝗘𝗠𝗔 𝗖𝗖𝗠 𝗜𝗡𝗔𝗞𝗘𝗠𝗘𝗔 𝗠𝗖𝗛𝗘𝗭𝗢 𝗠𝗖𝗛𝗔𝗙𝗨 𝗞𝗨𝗘𝗟𝗘𝗞𝗘𝗔 𝗨𝗖𝗛𝗔𝗚𝗨𝗭𝗜 𝗠𝗞𝗨𝗨
𝘼𝙩𝙤𝙖 𝙤𝙣𝙮𝙤 𝙩𝙖𝙗𝙞𝙖 𝙮𝙖 𝙠𝙪𝙩𝙚𝙣𝙜𝙚𝙣𝙚𝙯𝙚𝙖𝙣𝙖 𝙩𝙪𝙝𝙪𝙢𝙖 𝙯𝙖 𝙪𝙤𝙣𝙜𝙤 𝙞𝙡𝙞 𝙠𝙪𝙬𝙖𝙠𝙖𝙩𝙖𝙖 𝙬𝙚𝙣𝙮𝙚 𝙨𝙞𝙛𝙖 𝙯𝙖 𝙠𝙪𝙜𝙤𝙢𝙗𝙚𝙖.
𝘼𝙠𝙚𝙢𝙚𝙖 𝙠𝙪𝙩𝙤𝙖 𝙣𝙖 𝙠𝙪𝙥𝙤𝙠𝙚𝙖 𝙍𝙪𝙨𝙝𝙬𝙖 𝙠𝙬𝙖 𝙬𝙖𝙜𝙤𝙢𝙗𝙚𝙖 𝙣𝙖 𝙫𝙞𝙤𝙣𝙜𝙤𝙯𝙞 𝙬𝙖 𝙘𝙝𝙖𝙢𝙖.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Oganaizesheni, Ndg. Issa Ussi Gavu, amesema ni marufuku kufanya vitendo vichafu na vya uonevu ikiwemo kuzushiana tuhuma kwa lengo la kuwawekea vikwazo wenye lengo la kugombea uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Ndg. Gavu amesisitiza kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakitafumbia macho vitendo hivyo kwa kuwa kinataka wagombea watakaotokana na kura halali za ndani ya Chama ili kujihakikishia ushindi katika uchachaguzi huo.
Hayo ameyaeleza wakati alipokuwa na wanachama wa CCM Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam siku ya tarehe 14 Juni 2025 kwenye Kongamano la kumpongeza Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Katika hotuba yake, Ndg. Gavu ameendelea kuwahakikishia wana CCM wakiwemo wenye ni ya kugombea nafasi za ubunge na udiwani kuwa hakuna atakayekatwa kwa hila na uonevu.
Pia, alivitaka vikao vya uchujaji ngazi ya wilaya na mkoa kuhakikisha vinatenda haki kuwapitisha wenye sifa na wenye kasoro mbalimbali waitwe, wasikilizwe, wapewe nafasi ya kujieleza na ikibidi kuadhibiwa waadhibiwe kwa haki.
"Kwa hiyo ninachotaka kuwahakikishia ni kwamba Chama chetu mwaka huu wa uchaguzi tutahakikisha hakuna mtu atakatwa kwa sababu ya chuki hakuna, hakuna mtu wa kukatwa kwa sababu ya chuki hakuna, kama kuna mwanachama wa CCM kajaza fomu na mkajua ana upungufu mwiteni kwenye kikao mumuulize, mumhoji, halafu mfanye haki kwa kumpa alama anazostahili."
"Msifanye mambo ya kihuni, yapo mambo ya kukata kihuni kwa chuki zenu ama rushwa, unaonekana unajaza fomu ukaambiwa wewe ni mwizi ukaitwa katika kamati ya maadili ukifika pale katika kamati ya maadili unaulizwa jina lako nani...unasomeka wewe una tuhuma, tuhuma zako hujasomewa huzijui unaambiwa tu hivyo bila uthibitisho, utaratibu huo mara hii ukome."
Vilevile, Ndg. Gavu alitumia mkutano kuwatumia salamu kuwa CCM imedhamiria kutafuta viongozi wenye sifa, wasio na makandokando.
"Tuna wanachama zaidi ya milioni 13, nafasi za ubunge zipo nafasi 282, nafasi za udiwani zipo 4,030 kwenye kata na viti maalumu, hii maana yake nafasi moja ya ubunge ina watu zaidi ya 42,000, hatuwezi kukosa mtu mwenye sifa ndani ya watu 42,000 kwenda kutuwakilisha."
"Huu ni wakati wao wakachukue fonu tuwapime, tuwape nafasi, wanachama waamue na wanachama wakiamua tutawapa nafasi ya kupeperusha bendera ya chama chetu, lakini haiwezekani kuona mtu ametenga fedha zake na yeye anaamini kwamba CCM hii ataongoza."
#KaziNaUtuTunasongaMbele
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
09-12-2025
RAIS SAMIA AKIWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WATEULE- IKULU CHAMWINO DODOMA
09-12-2025
WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA (GENERAL)
09-12-2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ..
09-12-2025
RAIS SAMIA AKIHUTUBIA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
09-12-2025
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
09-12-2025
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
09-12-2025
𝗨𝗖𝗛𝗔𝗣𝗔𝗞𝗔𝗭𝗜 𝗪𝗔 𝗗𝗞𝗧. 𝗦𝗔𝗠𝗜𝗔 𝗨𝗠𝗘𝗟𝗘𝗧𝗔 𝗜𝗠𝗔𝗡𝗜 𝗞𝗪𝗔 𝗪𝗔𝗣𝗜𝗡𝗭𝗔𝗡𝗜, 𝗪𝗔𝗜𝗞𝗨𝗕𝗔𝗟𝗜 𝗖𝗖𝗠
𝙆𝙖𝙩𝙞𝙗𝙪 𝙈𝙠𝙪𝙪 𝘿𝙠𝙩. 𝙈𝙞𝙜𝙞𝙧𝙤 𝙖𝙬𝙖𝙥𝙤𝙠𝙚𝙖 𝙑𝙞𝙤𝙣𝙜𝙤𝙯𝙞 𝙬𝙖 𝘾𝙃𝘼𝘿𝙀𝙈𝘼 𝙣𝙖 𝘼𝘾𝙏
09-12-2025
𝗗𝗞𝗧. 𝗦𝗔𝗠𝗜𝗔 𝗔𝗧𝗨𝗔 𝗡𝗗𝗔𝗡𝗜 𝗬𝗔 𝗔𝗥𝗗𝗛𝗜 𝗬𝗔 𝗞𝗜𝗚𝗢𝗠𝗔
09-12-2025
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
09-12-2025
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
09-12-2025
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
09-12-2025
WANACHAMA 280 WA CHADEMA WATIMKIA CCM
09-12-2025
BALOZI NCHIMBI: MAONI YOYOTE KUHUSU AMANI YA TANZANIA HAYATAPUUZWA
09-12-2025
𝗦𝗘𝗥𝗜𝗞𝗔𝗟𝗜 𝗬𝗔 𝗥𝗔𝗜𝗦 𝗗𝗞𝗧. 𝗦𝗔𝗠𝗜𝗔 𝗜𝗠𝗘𝗪𝗘𝗞𝗔 𝗔𝗟𝗔𝗠𝗔 𝗬𝗔 𝗠𝗔𝗘𝗡𝗗𝗘𝗟𝗘𝗢 𝗞𝗜𝗟𝗔 𝗦𝗘𝗛𝗘𝗠𝗨 - 𝗖𝗣𝗔. 𝗔𝗠𝗢𝗦 𝗠𝗔𝗞𝗔𝗟𝗟𝗔
09-12-2025
MAKALLA: BARABARA YA MPWAPWA NJIAPANDA KONGWA KUJENGWA LAMI
09-12-2025
BALOZI NCHIMBI AWASILI ARUSHA
09-12-2025
TAARIFA KWA UMMA
09-12-2025
UCHAGUZI MKUU SIO AJALI-WASIRA
09-12-2025
𝗪𝗔𝗝𝗨𝗠𝗕𝗘 𝗠𝗦𝗜𝗖𝗛𝗔𝗚𝗨𝗘 𝗩𝗜𝗢𝗡𝗚𝗢𝗭𝗜 𝗟𝗘𝗚𝗘𝗟𝗘𝗚𝗘 𝗞𝗪𝗘𝗡𝗬𝗘 𝗞𝗨𝗥𝗔 𝗭𝗔 𝗠𝗔𝗢𝗡𝗜 - (𝗠𝗖𝗖) 𝗚𝗔𝗩𝗨
09-12-2025