Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla amesema Serikali ya Awamu ya Nane (8) kupitia Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2020-2025, Dira ya Maendeleo ya Zanzibar ya Mwaka 2050, Sera na Mikakati mbali mbali imekuwa ikiendelea kuimarisha Sekta ya Uwekezaji nchini kwa kuweka mazingira bora ambayo yanawavutia wawekezaji kuja kuekeza Zanzibar.
Ameyasema hayo katika hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Mradi wa Hoteli ya Mada yenye hadhi ya Nyota Tano (5) iliyoko Michanvi Kae Mkoa wa Kusini Unguja ikiwa ni katika shamra shamra za kutimia miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema kuwa Serikali inaendelea kuimarisha na kujenga miundombinu ya Barabara na Viwanja vya ndege sambamba na kuimarisha upatikanaji wa huduma za nishati, maji safi na salama na huduma nyengine za kijamii ili kuendelea kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji.
Mhe Hemed amefahamisha kuwa Mradi wa Ujenzi wa Hotel Mada unaomilikiwa na kampuni ya MADA HOTEL TANZANIA LIMITED hadi kukamilika kwake unatarajiwa kugharimu USD 6,500 utakaokuwa na vyumba mia moja(100) vya kulaza wageni na kusaidia kuzalisha ajira zaidi ya mia mbili (200) kwa vijana ambapo amewataka wawekezaji wa mradi huo kutoa kipaumbele cha ajira kwa wakaazi wa Michanvi na vijiji jirani.
Aidha Makamu wa Pili wa Rais amewasihi vijana ambao watapata ajira katika mradi huo kuwa waaminifu na kufanya kazi kwa bidii ili waendelee kuaminika katika majukumu watakayopangiwa sambamba na kuwataka wawekezaji wa mahoteli kutekeleza wajibu wao hasa katika kulipa kodi stahiki, kuwatendea haki wafanyakazi wao pamoja na kushirikiana na wananchi wanaoishi maeneo yanayowazunguka ili kudumisha amani na utulivu uliopo nchini.
Nae Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, kazi, Uchumi na Uwekezaji Mhe Mudrik Ramadhan Soraga amewataka wale wote waliopewa maeneo kwa ajili ya shuhuli za Uwekezaji kuyatumia maeneo hayo kama walivyopangiwa na Serikali na kuacha tabia ya kutoyatumia maeneo hayo na hatimae kuwa magofu jambo ambalo linarejesha nyuma malengo ya serikali.
Soraga amesema Sheria mpya ya uwekezaji ambayo inatarajiwa kusainiwa hivi karibuni imeainisha hatua zitakazochukuliwa kwa muwekezaji ambaye atazuwia eneo la uwekezaji pasipo kulifanyia shuhuli stahiki ikiwa ni pamoja na kurudishwa serikalini eneo hilo na kupewa wawekezaji wengine kwa maslahi ya taifa.
Amesema kuwa Mamlaka ya kukuza Uwekezaji Zanzibar(ZIPA) inafanya kazi kwa haraka na ufanisi mkubwa ili kuhakikisha upatikanaji wa huduma katika mamlaka hiyo unakuwa wa rahisi na kwa wakati muafaka.
Mapema Mkurugenzi Mtendajeji wa Mamlaka ya uwekezaji Zanzibar Ndugu sharif Ali Sharif amemshukuru muwekezaji kwa kuendelea kuiamini Zanzibar na kuja kufanya uwekezaji mkubwa ambao utatoa ajira nyingi kwa wazawa na kuipatia pato Serikali ya Zanzibari jambo litakalosadia katika kukuza uchumi wa Taifa letu.
Amesema mradi huo wa hoteli yenye hadhi ya nyota tano utagharimu jumla ya Dola milioni 30 na kutoa ajira zaidi ya watu 250 jaambo ambalo utakuza kipato cha mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Nae Muwekezaji wa Shukurani Palece Hotel Bwana TARLOCHAN MHANJAN amesema sababu kubwa ya kuja kuwekeza Zanzibar ni uzuri wa Visiwa vyenyewe na hali ya hewa inayopatikana, mazingira mazuri na ushirikiano wanaopatiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar sambamba na utayari wa wananchi wake kushirikiana na wawekazaji mambo ambayo yanawapelekea kufanya kazi zao kwa utulivu mkubwa.
Amesema kuwa Shukurani Palece Hotel inathamini na kuunga mkono Mapinduzi ya Zanzibar ambayo ndio msingi wa uwepo wa Amani na Utulivu uliosababisha uwepo wao hapa Visiwani Zanzibar.
MAFURIKO YA WANANCHI WA SIHA KWENYE MKUTANO MKUBWA WA HADHARA
30-05-2026
MAPOKEZI YA KATIBU MWENEZI WA CCM NDUGU KENANI L KIHONGOSI MKOANI KILIMANJARO
30-05-2026
🔰 𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈 𝐀𝐖𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐊𝐈𝐒𝐇𝐈𝐍𝐃𝐎 𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎
30-05-2026
CCM INAWATAKIA HERI YA SIKUKUU YA EID AL ADHA
30-05-2026
🔰VYAMA VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA VYAIMARISHA MSHIKAMANO, DKT. DIMWA AHITIMISHA MAFUNZO MAALUM
30-05-2026
KATIBU WA NEC, ITIKADI, UENEZI NA MAFUNZO CCM TAIFA NDUGU KENANI KIHONGOSI AMNADI MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ISIMANI EMMANUELA KAGANDA MTATIFIKOLO
30-05-2026
MUENDELEZO WA MAFUNZO YA VIONGOZI KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE – KIBAHA
30-05-2026
SIKU YA KWANZA YA MAFUNZO KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE LEADERSHIP SCHOOL.
30-05-2026
UFUNGUZI WA MAFUNZO YA VYAMA SITA RAFIKI VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA
30-05-2026
MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA MJUMBE WA KAMATI KUU YA CPC, KOMREDI LIU HAIXING IKULU DAR ES SALAAM
30-05-2026
KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CCM
30-05-2026
CCM NA FRELIMO KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIUCHUMI
30-05-2026
UZINDUZI WA JENGO LA MAKAO MAKUU YA ULINZI WA TAIFA
30-05-2026
CCM YAIPA POLE MSUMBIJI KWA KUKUMBWA NA MAFURIKO
30-05-2026
INJINI YA CHAMA CHA MAPINDUZI IPO MASHINANI; DKT.MIGIRO
30-05-2026
DK.MIGIRO:CCM INAJENGWA KUANZIA NGAZI YA MASHINA SIO MAJUKWAANI.
30-05-2026
𝗞𝗜𝗦𝗛𝗜𝗡𝗗𝗢 𝗖𝗛𝗔 𝗗𝗞𝗧. 𝗠𝗜𝗚𝗜𝗥𝗢 𝗖𝗛𝗔𝗣𝗢𝗞𝗘𝗟𝗘𝗪𝗔 𝗞𝗪𝗔 𝗦𝗛𝗔𝗡𝗚𝗪𝗘 𝗗𝗔𝗥 𝗘𝗦 𝗦𝗔𝗟𝗔𝗔𝗠
30-05-2026
NAIBU KATIBU MKUU WA CCM BARA AMWAKILISHA KATIBU MKUU WA CCM KWENYE MSIBA WA MBUNGE WA JIMBO LA PERAMIHO
30-05-2026
𝗩𝗜𝗝𝗔𝗡𝗔 𝗧𝗨𝗜𝗟𝗜𝗡𝗗𝗘 𝗔𝗠𝗔𝗡𝗜 𝗬𝗔 𝗡𝗖𝗛𝗜 𝗬𝗘𝗧𝗨 - 𝗠𝗪𝗘𝗡𝗘𝗭𝗜 𝗞𝗘𝗡𝗔𝗡𝗜
30-05-2026
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
30-05-2026