Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
PROF. KABUDI AWAFUNZA VIONGOZI VIJANA UMUHIMU WA KISWAHILI PAMOJA NA HISTORIA YA HARAKATI ZA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA
Prof Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi (Mb) ameshiriki Kutoa Mafunzo ya uongozi kwa Viongozi Vijana kutoka UWT na UVCCM, ambapo Leo tarehe 01 Novemba katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere amewafunza viongozi Vijana Umuhimu wa Lugha ya Kiswahili na namna Lugha yetu ilivyotumika kipindi cha Harakati za Kupigania Uhuru wa Nchi za Kusini mwa Afrika.
Pia Prof. Kabudi amewafunza namna Mwalimu Nyerere alivyopambana kuhakikisha Tanzania tunakuwa wa moja kama nchi licha Kutofautina Makabila na kutufanya nchi za Africa kwa Pamoja kuzungumza lugha moja ya Kiswahili.
Mafunzo haya ya viongozi vijana 50 kutoka UWT na UVCCM yenye lengo la kuwaanda viongozi vijana ambao watakwenda kulitumikia taifa Pamoja chama na kuwafanya Vijana hao Kuwa Mabalozi wazuri kwa kuwafundisha vijana wenzao elimu waliyoipata kwenye Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere iliyopo Kibaha, Mkoa wa Pwani
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.