Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
RAIS SAMIA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA MSUMBIJI MHE. FILIPE JACINTO NYUSI.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan aongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo Rasmi na Mgeni wake Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Julai, 2024.
Aidha, Rais Samia akizungumza na Waandishi wa Habari Ikulu Jijini Dar es Salaam kuhusiana na Ziara ya Kiserikali ya Mgeni wake Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi wameshuhudia utiaji saini Hati ya Makubaliano ya kushirikiana katika masuala mbalimbali baina ya Tanzania na Msumbiji ikiwemo Afya na Uwekezaji.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.