RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK.HUSSEIN MWINYI AHUTUBIA MAADHIMISHO YA MIAKA 25 YA ZSSF
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amemuagiza Mkurugenzi mwendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) kuwasilisha kwake orodha ya majina ya waajiri wasiowasilisha michango ya waajiiriwa wao kwenye Mfuko huo ili awachukulie hatua kwaajili ya kulinda haki za watu.
Dk. Mwinyi alitoa agizo hilo ukumbi wa hotel ya Golden Tulip, uwanja wa ndege, Mkoa wa Mjini Magharibi kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa ZSSF. Alisema, kazi kubwa inayoendelea kufanywa na ZSSF ni mabadiliko na huduma bora kwenye sekta ya uwekezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo inayogusa jamii moja kwa moja. “Miradi yote inayotekelezwa na iliyopangwa kutekelezwa na ZSSF sina shaka itaongeza faida kwa ZSSF, itakuza uchumi na kutoa fursa nyingi za ajira nchini” Alisifu Rais Dk. Mwinyi.
Alisema, ZSSF inatokana na ushirikiano baina ya Serikali, Waajiri na Waajiriwa, hivyo alizitaka taasisi za Serikali na Jumuiya zote kuwasilisha michango yao kwa wakati ili kurahisisha shughuli za uendeshaji wa taasisi hiyo kwa lengo la kuwajengea misingi mizuri wafanyakazi wao wanapostaafu au wanapohitaji mafao yao. Pia Rais Dk. Mwinyi alizitaka Taasisi za Serikali zishirikiane kutoa huduma ili kuwaondolea usumbufu usio wa lazima wananchi.
Kadhalika, aliwaomba wajasiriliamali wajisajili ili wachangia kwenye Mfuko wa hiari kwani una faida hasa pale biashara zao zitakapotetereka au watakapohitaji mafao ya aina yoyote. Akitoa ushuhuda kwa mataifa yaliyoendelea duniani, Rais Dk. Mwinyi alieleza lengo la kuanzishwa kwa sekta za huduma za jamii ni kukusanya michango, kuwekeza na kulipa mafao kwa mujibu wa sheria zilizopo.
Aidha, alieleza Sekta hiyo pia hutumika kuinua uchumi wa nchi na wananchi hasa kwenye uwekezaji wa miradi mikubwa yenye tija. Alisistiza, Sekta ya hifadhi ya jamii ni nguzo muhimu ya uchumi inayotegemewa na nchi pamoja na wafanyakazi. Alieleza licha ya mafanikio makubwa ya ZSSF ndani ya miaka 25 tokea kuanzishwa kwake, lakini bado haijawekeza kwenye miradi mikubwa zaidi, hivyo, aliieleza taasisi hiyo ina wajibu wa kujifunza kwa wengine ili kuongeza ufanisi kwenye uwekezaji wenye tija zaidi.
Pia, aliipongeza ZSSF kwa utekelezaji wa agizo lake la kuongeza pensheni kwa wastaafu wa kima cha chini kutoka shilingi 90,000 hadi 180,000 kama Serikali ilivyoongeza kwa wastaafu wanaolipwa kupitia Wizara ya Fedha. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango, Dk. Saada Mkuya Salum, alieleza malifakutoa mafao kwa wastaafu lakini pia ZSSF imegusa hudua zote za jamii zikiwemo, Afya michezo, elimu vituo vya daladala na huduma nyengine kwa wananchi.
Naye, Mkurugenzi Mwendeshaji Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar, Nassor Shaaban, alieleza lengo la kuunzishwa kwa Mfuko huo ni kutoa ulinzi na kinga kwa wanachama wake kwa kutoa pencheni na mafao mbalimbali. Akizungujmzia mafanikio ya ZSSF kwa kipindi cha miaka miwili ya Dk Mwinyi alieleza ni pamoja na utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2025 nakuonengeza hadi sasa Mfuko umetekeleza miradi ya maendeleo kwa asilimia 90, pamoja na kutekeleza jukumu la kisheria la mfuko ikiwemo kusajili mwanachama, uwekezaji pamoja na ulipaji wa mafao na pencheni.
Miongozi mwa mafao yanayotolewa na ZSSF ni pamoja fao la kustaafu, uzazi, fao la wenye ulemavu, kuumia kazini na fao la wajasiriamali. ZSSF ilianzishwa rasmi mwaka 1998, maadhimisho ya miaka 25 ya taasisi hiyo yalikwenda sambamba na kauli mbiu, “Nidhamu, Uwajibikaji teknolojia ya sasa na uwekezaji endelevu na mafao bora kwa wanachama”.
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
09-12-2025
RAIS SAMIA AKIWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WATEULE- IKULU CHAMWINO DODOMA
09-12-2025
WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA (GENERAL)
09-12-2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ..
09-12-2025
RAIS SAMIA AKIHUTUBIA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
09-12-2025
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
09-12-2025
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
09-12-2025
π¨ππππ£πππππ πͺπ πππ§. π¦ππ ππ π¨π ππππ§π ππ ππ‘π ππͺπ πͺππ£ππ‘πππ‘π, πͺππππ¨ππππ πππ
πππ©πππͺ ππ πͺπͺ πΏπ π©. πππππ§π€ ππ¬ππ₯π€π ππ πππ€π£ππ€π―π π¬π πΎππΌπΏπππΌ π£π πΌπΎπ
09-12-2025
πππ§. π¦ππ ππ ππ§π¨π π‘πππ‘π π¬π ππ₯πππ π¬π ππππ’π π
09-12-2025
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
09-12-2025
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
09-12-2025
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
09-12-2025
WANACHAMA 280 WA CHADEMA WATIMKIA CCM
09-12-2025
BALOZI NCHIMBI: MAONI YOYOTE KUHUSU AMANI YA TANZANIA HAYATAPUUZWA
09-12-2025
π¦ππ₯πππππ π¬π π₯πππ¦ πππ§. π¦ππ ππ ππ ππͺπππ ππππ π π¬π π πππ‘πππππ’ ππππ π¦ππππ π¨ - ππ£π. ππ π’π¦ π ππππππ
09-12-2025
MAKALLA: BARABARA YA MPWAPWA NJIAPANDA KONGWA KUJENGWA LAMI
09-12-2025
BALOZI NCHIMBI AWASILI ARUSHA
09-12-2025
TAARIFA KWA UMMA
09-12-2025
UCHAGUZI MKUU SIO AJALI-WASIRA
09-12-2025
πͺπππ¨π ππ π π¦ππππππ¨π π©ππ’π‘ππ’ππ ππππππππ ππͺππ‘π¬π ππ¨π₯π ππ π ππ’π‘π - (π ππ) πππ©π¨
09-12-2025