Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


MWENEZI MAKALLA AANZA ZIARA YA KUTEMBELEA VYOMBO VYA HABARI, AELEZA MAKUBWA YANAYOFANYWA NA RAIS DKT. SAMIA KATIKA MIRADI YA MAENDELEO NCHINI 

alternative

> Agusia mchakato wa Katiba Mpya 

> Asema kupitia ziara iliyofanyika hivi karibuni ya Katibu Mkuu Dkt. Nchimbi, CCM imetatua kero 160 za wananchi 

> Asema CCM inaendelea kutambua na kuheshimu muhimili wa mahakama hivyo haitajihusisha na utatuzi wa kesi ambazo tayari zipo mahakamani 

Katibu wa NEC - Itikadi,Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa Ndugu. Amos Makalla, ametembelea studio za Azam Media Limited na Mwananchi Communications Limited (MCL) ikiwa ni kuanza kwa ziara yake ya kutembelea vyombo mbalimbali vya habari hapa Nchini.

Akizungumza kwenye mahojiano katika kipindi cha #MorningTrumpet cha UTV  pamoja na waandishi na wahariri wa kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) , Mwenezi Makalla ameeleza sababu za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuingia mitaani kusikiliza na kutatua kero na changamoto za Wananchi.

Mwenezi Makalla ameeleza kazi kubwa inayofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji wa kasi wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo nchini ikiwemo Bwawa la kufua umeme la Mwl. Nyerere, Mradi wa Reli ya kisasa ya SGR, Miradi ya Elimu, Afya na Miundombinu ya Barabara pamoja na viwanja vya ndege.

Sambamba na hayo, ameeleza namna mchakato mzuri unavyoendelea kufanyika kuhusiana na upatikanaji wa katiba mpya kwa kuzingatia taratibu ya kuchukua maoni ya wananchi na si maoni ya vyama vya siasa pekee.

Aidha, Makalla amesema tuhuma zinazotolewa na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu kuhusu kuwepo kwa fedha chafu zinazoingizwa ndani ya chama chao ili kuwavuruga si za kweli na kusema saula hilo si la kuupuziwa hivyo kumuomba msajili wa vyama vya siasa na TAKUKURU kufanya uchunguzi wa tuhuma hizo.

🗓️7 Mei, 2024
📍Jijini Dar es salaam

alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine

Nukuu za Viongozi