Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
MKUTANO WA NDANI MKOA WA KILIMANJARO KATIKA ZIARA YA KATIBU MKUU DKT.NCHIMBI
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk Emmanuel John Nchimbi, katika Mkutano wa ndani akizungumza na Wanachama na Viongozi wa Chama na Serikali na wawakilishi wa makundi mbalimbali Mkoa wa Kilimanjaro katika Ukumbi wa ofisi za CCM mkoa wa Kilimanjaro leo Juni 5,2024.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.