Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
KATIBU MKUU WA CCM BALOZI DK NCHIMBI AKATISHA ZIARA YAKE YA KIKAZI NCHINI INDIA KUSHIRIKI MSIBA WA HAYATI ALHAJ ALI HASSAN MWINYI.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi akisalimiana na Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania, Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir Bin Ally, walipokutana Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Abeid Amani Karume. Dk. Nchimbi amewasili Zanzibar leo Jumamosi, Machi 2, 2024, akitokea nchini India, ambako amelazimika kukatisha ziara yake ya kikazi, kushiriki msiba wa Mwenyekiti wa CCM Mstaafu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mstaafu wa Awamu ya Pili, Hayati Alhaj Ali Hassan Mwinyi.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.