Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


DKT NCHIMBI AHANI MSIBA WA ALIYEKUWA  MWENYEKITI WA CCM BARIADI 

alternative

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, akiambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Ndugu Amos Gabriel Makalla na Katibu wa NEC - Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Ndugu Rabia Hamid Abdalla, amefika kuwapatia pole familia ya Bi. Juliana Wilemahongo, aliyefariki dunia tarehe 15 Septemba 2024. Bi Wilemahongo hadi anafikwa na mauti, alikuwa ndiye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bariadi, akiwa amejitolea kutumikia nafasi hiyo ya uongozi kwa vipindi vitatu.

alternative alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine

Nukuu za Viongozi