Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR AFUNGUA MAFUNZO KWA VIONGOZI WA UWT NA MADIWANI WANAWAKE UNGUJA-ZANZIBAR
Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Hemedi Suleiman Abdullah Leo tarehe 11 Mei, 2024 amefungua Mafunzo kwa viongozi wa UWT na Madiwani Wanawake Unguja Zanzibar yaliyofanyika katika ukumbi wa Nyamazi, Dimani Zanzibar
Mafunzo hayo yametolewa kwa makatibu wa UWT ngazi ya Wadi,Majimbo pamoja na Madiwani Wanawake wa Kuteuliwa Unguja- Zanzibar.
Viongozi Mbalimbali wakiongozwa na Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC), Makamu wa Mwenyekiti wa UWT Ndg. Zainab Khamis Shomari (MNEC), Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Magharib Ndg. Mohamed Rajab, Wajumbe wa Halmashauri Kuu Ya CCM Taifa kutoka UWT, Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Mgeni Hassan Naibu Katibu Mkuu wa UWT-Zanzibar Ndg. Tunu Kondo Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji la Baraza Kuu la UWT, pamoja na Baadhi Wajumbe baraza kuu la UWT Wamehudhuria Mafunzo hayo.
📍 Unguja, Zanzibar
🗓️ 11 Mei, 2024
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.