Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


MAKAMU WA PILI WA RAIS ALHAJJ HEMED SULEIMAN ABDULLA AMEWATAKA WANANCHI KUZINGATIA MAELEKEZO YANAYOTOLEWA NA WATAALAMU WA HALI YA HEWA HASA KATIKA KIPINDI HICHI CHA MVUA ZA VULI ZINAZOENDELEA KUNYESHA NCHINI.

alternative

Alhajj Hemed ameyasema hayo alipokuwa akiwasalimia waumini wa Masjid LILLAH  kianga   Wilaya ya Magharibi  "A" mara baada ya kumaliza  Ibada ya sala ya Ijumaa.

Amesema imekuwa ni utamaduni wa wananchi wa Zanzibar kujisahau na kufanya shuhuli za ujenzi wakati wa jua kali  sehemu ambazo sio sahihi kwa makaazi ya watu na kupelekea kuhangaika na familia wakati wa mvua kali zinaponyesha jambo ambalo huleta usumbufu mkubwa  kwa baadhi ya wananchi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  amesema ili kujinga na maafa hasa katika kipindi hiki cha Mvua zinazoendelea kunyesha ni vyema wananchi kuacha kujenga  nyumba za makaazi sehemu ambazo sio salama pamoja na wale wanaoziba njia za maji jambo ambalo hupelekea athari kubwa kwa wananchi  wakati wa mvua  kubwa.

Alhajj Hemed ametoa pole kwa wale wote ambao wamepatwa na maafa kutokana na  mvua kubwa  iliyonyesha mwishoni mwa wiki iliyopita na kuwataka wananchi kuweza kusaidiana pale mmoja wao anapopatwa na tatizo la aina yoyote  ikiwemo la maafa.

Aidha Makamu wa Pili wa Rais  wa Zanzibar amesema Serikali ya Awamu ya Nane (8) inayoongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Alhajj Dkt. Hussein Ali Mwinyi itahakikisha inatoa ushirikiano na msaada wa hali ya juu kwa mwananchi yeyote atakaepatwa na tatizo la aina yoyote ikiwemo la maafa.

Sambamba na hayo Alhajj Hemed  amewasisistiza waumini wa Msikiti huo na wananchi kwa ujumla kuzidisha  kudumisha amani, upendo na ushirikiano katika jamii ili nchi iweze kupata maendeleo.

Hata hivyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewaomba waumini kuendelea kuunga mkono juhudi zinazochukuliwa na Serekali za kuwaletea maendeleo wananchi wake  kwani Serikali inajenga miradi mingi ya kimkakati ambayo itakuwa na tija kwa vizazi vya sasa na baadae.

Mapema akitoa Khutba katika Sala ya Ijumaa, Maalim Suleiman Hamad Suleiman  amewataka waumini kushirikiana pamoja na kupeana elimu juu ya maisha ya ahera jambo ambalo wengi wao mamejisahau kuwa maisha ya dunia ni mapito tu.

Amesema ni wajibu wa  waumini kumlingania mwenzake kwa kutumia lugha nzuri ili kuondosha mifarakano inayoweza kutokea pamoja na kuwataka waumini kutafuta  chumo la halali katika kipato chao cha kila siku ili kujiwekea maisha yaliyobora mbele ya allah.

alternative alternative
Habari Nyingine

Nukuu za Viongozi