Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
RAIS SAMIA AZINDUA RASMI SAFARI ZA TRENI YA KISASA (SGR) DAR - DODOMA.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Ndg. Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua rasmi safari za Treni ya Kisasa (SGR) kutoka Dar Es Salaam - Dodoma, leo Agosti 1,2024 katika Stesheni ya SGR jijini Dar Es Salaam.
Uzinduzi huo ukishuhudiwa na Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali pia wakiwemo wasanii na wananchi lukuki.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.