GEITA MJINI IMEITIKA! MKUTANO WA KATIBU MKUU WA CCM.
Mkutano wa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi katika uwanja wa Shule ya Msingi Uwanja Geita Mjini ambapo amezungumza na Wanachama wa chama hicho na Wananchi wa Mkoa wa Geita leo tarehe 13 Agosti 2024.
Katika mkutano huo katibu Mkuu aliambatana na Manaibu waziri watatu kutoka wizara za Tamisemi, Mambo ya Ndani ya Nchi pamoja na Ujenzi.