CCM YAWAONYA WANAO JIPITISHA MAJIMBONI, UTEUZI NA UTENGUZI YA WAJUMBE
Katibu wa NEC, Itikadi Uenezi na Mafunzo CCM, Amos Makalla ametoa maelekezo kwa watendaji wa chama hicho ngazi zote nchini kuanza kuwabaini makada wanaoanza kujipitisha pitisha majimboni kwenye Kata kalba ya wakati kwa lengo la kujitengenezea mazingira ya kusaka vyeo.
CPA. Makalla ametoa maelekezo hayo leo Jumanne Machi 4, 2025 kwenye mkutano wake wa ndani wa viongozi wa Chama hicho, Jumuiya ngazi ya Shina, tawi, mitaa, Kata na Wilaya ya Kinondoni uliofanyika Ukumbi wa Kiramuu Mbezi Shule ikiwa ni mwanzo wa ziara yake ya siku nne aliyoanza kwa mkoani Dar es salaam.
Dhima ya mkutano huo CPA. Makalla kama mlezi wa mkoa huo kichama ulilenga kuwahamasisha viongozi hao kuhamasisha umma kujitokeza kwa wingi kwenye shughuli ya uboreshaji ya taarifa kwenye daftari la mpiga kura ambalo kwa mkoa huo linatarajiwa kuanza Machi 17 hadi 23 mwaka huu.
Pia amesema watendaji hao wanapaswa kuanza shughuli ya kuwabaini sasa ili kuwalinda wanaoshikilia nafasi hizo Wabunge na madiwani waachwe wafanye kazi zao kwa uhuru.
"Wanaojipitisha pitisha rekodi zenu zinatinazwa naagiza makatibu na watendaji wote muwabaini tutazitumia orodha hizo kwenye kufanya mchujo wa wagombea, Waliopo sasa ni wabunge madiwani wetu waachwe wafanye kazi hadi muda wao utakapofika," amesema
Aidha, Amesema Wabunge wanajiandaa kwenye bunge la bajeti ni lazima muealinde kwa sababu wanabeba maono ya wananchi haiwezekani wanaendelea na shughuli hiyo lakini jimboni kuna mwingine unakazana kwenye eneo lake kujiouza.
"Kumekuwa na fitina fitina na fitina mtu anakuja gia ya kwanza Mbunge wenu mara ya mwisho mlimuona lini huku unajua kabisa kuna kamati za maendeleo inakuwaje wewe unauliza swali la namna hiyo ni fitina ya bure," amesema
Kulingana na Makalla amesema baada kuona mtindo huo unakuja kwa kasi aliwaelekeza watendaji na Kamati za siasa kuweka rekodi za watu wote wanajipitisha na kufanya kampeni kwani watawarahisishia kwenye mchujo ili wasipigiwe kura za maoni.
"Ndugu zao hatutanini na bahati isiyokuwa nzuri Dar es Salaam mimi ni mlezi wa mkoa huu kwahiyo muda ukifika nafasi zipo mtaomba lakini kwa sasa naelekeza muache kuwasumbua wabunge na madiwani wafanye kazi zao,"
Katika maelezo yake amesema ni muhimu wakaa kimya waendelee kuusoma mchezo huku akisema mara nyingi samaki anayeangaika muda wote ndiye ananaswa kwenye ndoana.
"Kuna watu wamejiweka weka kukamatwa na ndoana sasa hatutakuwa na huruma kwenye mchujo wa kura za maoni,":amesema
Mbali na hilo, Makalla ametoa amelekezo kwa Watendaji kusimamia kuhakikisha mtindo ulioibuka wa kuteua na kutengua mabalozi wa serikali za mitaa unakoma unaofanya na baadhi ya viongozi ili kujitengenezea safu.
"Natoa maelekezo kwa Makatibu ngazi zote kuweka kukemea baadhi ya viongozi wanaofanya kazi ya kupangua kuweka mabalozi wapya kumbukrni walishachaguliwa alafu mtu anapita kupangua nakusema tuweke tunaoendana nao, haiwezekani jambo hilo Mabalozi waliotusaidi na tukashinda serikali za mitaa wapanguliwe,"
Amesema chama hicho hakitaki kuona jambo hilo likifanyika na wanajua wanaotenda mchezo huo ni kwa sababu ya utashi wa baadhi ya watu wenye uchu wa madaraka wakitaka kupanga safu kwa uchaguzi ujao.
"Mabalozi wakati nawatetea nayie mchangamke msiniangushe baada ya tamko hili msikibali kutenguliwa hawezekani suala la uteuzi na utenguzi liendelee kufanyika nawakemea watendaji lakini nayie nawaomba msiwakane watu wenu endeleeni kushirikiana nao,"
Kuliangana na Makalla amesema jambo hilo kupangua na kuteua mabalozi waliligundua baada ya kupata taarifa kutoka Wilaya moja ambayo hakutaka kuiweka wazi katika mkutano huo wa ndani.
"Baada ya kupata taarifa hilo tuliwaandikia barua kali ya onyo kuwaonya, lazima mjue chama chetu kimeamua kuongeza watu wa kushiriki kupiga kura za maoni kwa lengo la kukuza demokrasia lakini kuondoa mianya ya rushwa, "
#CCMImara
#VitendoVinaSauti
#KaziIendelee