Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
RAIS DK.MWINYI AWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU ALIOWATEUA.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amewataka viongozi mbalimbali kuongeza kasi mara mbili kuwatumikia wananchi pamoja na kukamilisha ahadi na kuvuka utekelezaji.
Rais Dk.Mwinyi amesema hayo katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri wapya aliowateua hivi karibuni viwanja vya Ikulu Zanzibar tarehe: 01 Februari 2024.
Aidha Rais Dk.Mwinyi amemtaka Waziri wa utalii na mambo ya kale Mhe.Mudrick Ramadhan Soraga kuweka juhudi kubwa kupanua wigo katika Sekta ya Utalii hususan utalii wa urithi, mikutano na michezo.
Vilevile, Rais Dk. Mwinyi amemtaka Waziri mpya wa Wizara ya Uchumi wa Buluu Mhe. Shaaban Ali Othman kuongeza juhudi katika kuzitatua changamoto za wananchi na kukuza vipato vyao pamoja na fursa za mafuta na gesi katika sekta hiyo.
Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amewaagiza Wizara ya ardhi kutatua migogoro ya ardhi.
Rais Dk.Mwinyi amesema Kujiuzulu kwa Waziri si jambo geni ni njia ya uwajibikaji, ameeleza kuwa wakati una wajibika kujiuzulu lazima kuwa mkweli kama kuna sababu za mgongano wa kimaslahi utangaze na kusema wazi sababu zilizokufanya uwajibike
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.